November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake jitokezeni kuwania uongozi uchaguzi serikali za mitaa

Na Daud Magesa, Timesmajira Online,Magu

WANAWAKE wameshuriwa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.


Ushauri huo umetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza,Elizabert Nyingi,wakati akizungumza na wajumbe (mabalozi) wa shina namba 017,Kisesa Kata ya Bujora,wilayani Magu, ikiwa ni kuadhimisha miaka 47 ya CCM.

Amesema uchaguzi wa serikali za mitaa utakofanyika mapema mwaka huu,wanawake wajitokeze kuomba na kugombea nafasi za uongozi kwa kuwa tayari wamepewa kuongoza nchi kuangalia kama wanaweza ama hawawezi ambapo majibu yake yanaonekana.

“Tunaongozwa na Mama Jemedari wetu Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,ameonesha uwezo mkubwa wa uongozi wa nchi na hivyo nawasihi akinamama wenzangu msibaki nyuma,ombeni nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa tumuunge mkono Rais na Mwenyekiti wetu wa CCM,”amesema Nyingi.

Pia amesema licha ya kujitoa kuomba kuchaguliwa na kupiga kura washirikiane na wanaume ambao ni vichwa vya familia kuhakikisha CCM inapata ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa, mwaka huu ambapo utaonesha taswira ya kazi aliyoifanya Rais Dkt.Samia.

Nyingi amesema wana CCM wanapaswa kuhamasisha wasio na kadi wajiunge na wasajiliwe katika mfumo wa kielektroniki kwa kulipia kadi sh.2,000 na ada ya sh. 1,200 na wawahamasishe hata wa vyama vingine na wasio na vyama wajiunge na CCM.

“Twendeni tujipange,haya tunayoyafanya ni maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kuhakikisha vijiji,vitongoji na mitaa yote CCM inashinda,”amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa shina namba 017, Felister Mwandu,amesema Rais Samia aliachiwa na kuubeba mzigo mzito wa kuleta maendeleo ya wananchi.