May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mhandisi kutoka Chuo cha Ualimu cha VETA mkoani Morogoro Frank Urio akielekeza jambo mara baada ya kutembelea kwenye Banda lao Sabasaba mkoani Dar es Salaam

Wanaosoma faini ya umeme washauriwa kutembelea banda la VETA Sabasaba

Na David John,TimesMajira Online

WANAFUNZI wanaosoma umeme wametakiwa kujitokeza kwenye viwanja vya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa na kutembelea kwenye banda la Chuo cha Ualimu cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (MVTTC EETA MOROGORO)ili kupata elimu kuhusu umeme

Mhandisi Frank Urio akiwa kwenye Picha ya pamoja na mkufunzi Mwandamizi wa Chuo hicho Sophia Tuka kulia na kushoto ni miongoni mwa walimu

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye viwanja hivyo Frank Urio ambaye ni mhandis kutoka chuo hicho kilichopo mkoani Morogoro amesema kuwa wapo katika maonyesho hayo na wamekuja na kifaa kipya kuhusu umeme.

Amesema kuwa kuna changamoto kubwa sana kwa wanafunzi ambao wanakwenda kufanya mafunzo kwa vitendo na ndio maana kupitia maonyesho hayo wamekuja na kifaa hicho ili kuwapa elimu sahihi kwani ni teknolojia mpya na ndani yake kuna mafunzo ya aina mbili ambayo ni electronic mashine na nyingine.

“Ndugu waandishi kikubwa kupitia maonyesho haya tunawaomba wanafunzi wajitokeze kwa wingi ili waje kupata elimu stahiki kuhusu umeme na kama mnvyojua changamoto za umeme kwa hiyo tupo hapa hadi Julai 13 hivyo wajitokeze,”amesema mhandisi Urio

Ametoa wito kwa wanafuzni ambao wamesoma umeme waje ili wafundishwe kujua namna ya kuona vifaa hivyo jinsi vinavyofanya kazi ili akiwa katika maeneo yake ya kazi asikutane na changamoto kubwa.

Naye Sophia Tuka ambaye ni mkufunzi mwandamizi chuoni hapo akizungumzia kozi ambazo zinatolewa chuoni hapo hususani mwaka huu wa masomo amesema kuwa chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali za ualimu na wanaandaa walimu wanaofundisha ufundi.

Amesema katika chuo chao wanatoa elimu ya ufundi katika ngazi ya cheti na pia wanatoa mafuzo kwa ngazi ya astashahada (Diploma) na mwezi wa tisa masomo yanaaza hivyo wanafunzi wajitokeze na kujiunga ili kuweza kupata elimu ya ufundi.

“Ndugu zangu wanahabari pia katika chuo chetu Tuna kozi ya postgraduetu ambayo  imesajiliwa na TCU na tunashirikiana na nchuo kikuu huria na kimsingi tuna muhula wa mwezi wa tisa na nyingine itakuwa ya awamu ya pili “amsema Tuka.