Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
KUELEKEA Mashindano ya Mbeya Tulia Marathon wananchi na wadau wameombwa kujitokeza kujisajili katika mashindano hayo ili kuonyesha kujali shughuli za kijamii ambazo zimekuwa zikifanywa na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini na Spika wa Bunge na Rais Umoja wa Mabunge Duniani Dkt.Tulia Ackson lengo likiwa ni uboreshaji wa miundombinu ya afya pamoja na elimu.
Kauli hiyo imetolewa Mei 7,2024 na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya DorMohamed Issa wakati alipofika katika Uwanja wa Sokoine Jijini hapa kutembelea na kuona maandalizi wa uwanja huo kwa ajili Mashindano ya Mbeya Tulia marathon yanayotarajiwa kufanyika Mei 10 mpaka 11 ,2024 ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa.
“Niwaombe wana Mbeya sisi ni wenyeji wamashindano haya Mgeni rasmi anatajarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa niwaombe wana Mbeya kwa mshikamano wenu tujitokeze kwa wingi kuona kile kinachofanywa na Mbunge wetu cha kuwaletea maendeleo wananchi”amesema Meya Issa.
Hata hivyo Issa alimshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusapoti michezo na kupenda pia alimshukuru Rais umoja wa mabunge duniani na Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson kwa kazi kubwa ambazo amekufanya kwa lengo la kuhamasisha kwa kuleta matukio mkoani hapa mara kwa mara yenye dhana njema yenye lengo la kudumisha afya umoja na mshikamano ,safari hii tunaingia kwenye mashindano ya Tulia Marathon kwa msimu wa saba ambapo Dkt.Tulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust.
Aidha Issa amesema kuwa mambo ambayo amekuwa akifanya Dkt.Tulia katika Jiji la Mbeya ni katika kuhakikisha kuwa mkoa huu unaamka lakini yeye kama Mbunge kuwa karibu na wananchi kupitia dhana ya michezo,utamaduni na vitu vingine muhimu katika jamii na kusema kuwa fedha zote ambazo zinapatikana kupitia mashindano ya Tulia Marathon amezielekeza kwenye uboreshaji wa miundo ya afya ,elimu na kuwa hilo ni jambo kubwa kwa Jiji letu la Mbeya .
Hata hivyo amewaomba viongozi wa kata, Mabarozi,Matawi ,Madiwani pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi katika usajili wa mashindano hayo na mapokezi ya waziri wa mkuu ili kuonyesha kuwa mbeya tupo na ushirikiano wa kutosha upo.
Kwa upande wa wake Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust ,Joshua Mwakanolo amesema Aprili 7,2024 wamepokea viongozi wa kamati ya siasa wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM),Afrey Nsomba kwa ajili ya kujisajili mashindano ya Mbeya Tulia Marathon ambapo fedha zinazopatikana baada ya mashindano Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson huzielekeza kwenye uboreshaji wa miundo mbinu ya afya na elimu katika Jiji la Mbeya.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba