May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wananchi Kata ya Mzimuni waridhishwa na utendaji kazi wa Diwani

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

BAADHI ya Wananchi wa Kata ya Mzimuni Wilaya ya Kinondoni wamesema wanaridhishwa na Utendaji kazi unaofanywa na Diwani wa Kata hiyo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Manifred Lyoto kwa kuwaletea maendeleo.

Maendeleo hayo ni katika sekta ya afya,elimu,michezo na miundombinu ya Barabara na Maji.

Pongezi hizo wamezitoa Jijini Dar es salaam wakati wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kata hiyo kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi,ambapo wamesema kata hiyo imepiga hatua kubwa kimaendeleo.

Mmoja wa wananchi hao anayefahamika kwa jina la Abdallah Kitumbi Mkazi wa Mtaa wa Mtambani alisema kuwa Diwani huyo ni kiongozi wa kuigwa kwani ameboresha sekta ya Elimu kwa kuhakikisha amejenga Uzio wa Shule ya Sekondari na Msingi Mzimuni ,ameweka Miundombinu ya kuwezesha Wanafuzni kupata chakula Shuleni,ameajiri walimu wa masomo ya sayansi hatua ambayo imechangia kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi.

“Wazazi wanatoa elfu moja tu ya chakula kwa watoto wao ,Miundombinu mingine yote kama vile Jiko,Masufuria,Kontena la kuhifadhia chakula vyote amechangia Diwani kupitia fedha zake mwenyewe ili kuwapunguzia mzigo wa michango wananchi wa Mzimuni,kwakweli amekuwa akijitoa sana kutatua kero za wananchi”amesema Kitumbi.

Kwa upande wake mkazi wa mtaa wa Mwanansari Irene Mwakingila amesema kuwa Diwani huyo amefanikiwa kutatua chagamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakumba.

“Tunawashukuru sana kiongozi wetu kwani kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kutatua chagamoto mbalimbali ambazo tulikuwa tukikumbana nazo ikiwemo kuboresha huduma za afya katika Zahanati ya Mzimuni kutokana na kuoneza watumishi wengine wa afya kwenye Zahanati hiyo ili kuhudumia wakazi wa maeneo hayo na kata jirani”alisema.

Aliongeza kuwa Diwani huyo ameanzisha Taasisi ya kutoa Mikopo isiyokua na riba kwabajili Makundi ya Wajasiliamari ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi,ambapo Taasisi hiyo iitwayo “Lyoto Foundation” itaanza kutoa mikopo kuanzia Mwezi Julai mwaka huu.

Naye Kassim Kinguyu Mkazi wa Mtaa wa Mtambani amesema Sekta ya Michezo nayo amefanikiwa kuiinua kwani tayari baadhi ya timu za vijana zimepatiwa vitendea kazi vya Michezo ikiwemo Jezi na Mipira.

Amesema kuwa kwa sasa yupo katika Mazungumzo na wataalamu wa soka kutoka Mataifa ya Nje kwa ajili ya kuwapeleka vijana wenye vipaji kufanyiwa majaribio ya kucheza soka la Kimataifa.

Awali Diwani wa kata ya Mzimuni Manifred Lyoto alisema ameamua kujitoa kuwasaidia Wananchi wa Kata hiyo ikiwa ni ahadi ya kutimiza adhma ya serikali ya sita ya kazi iendelee.

Amesema Serikali peke yake haiwezi kufanya mambo yote kwa wakati Mmoja kutokana na kuendelee kutekeleza miradi mingi ambayo inahitaji fedha nyingi.

“Serikali ina mambo mengi yakufanya ,ina miradi mikubwa inayohitaji fedha,hivyo sisi kama wawakilishi wa wananchi kama tunaweza kusaidia kupitia vyanzo vyetu vya binafsi vya Mapato au kutafuta wadau wa kusaidia haina budi kufanya hivyo ili kuinga mkono serikali katika kuwaletea Wananchi Maendeleo “amesema Lyoto

Aidha aliwaomba Wananchi wa kata hiyo kuwa na mwamko wawe na mwamko mkubwa wa kupeleka watoto wao shuleni kwani tayaru chagamoto ya ukosefu wa shule imetatuliwa.

Akizungumzia kuhusu utoaji wa Mikopo kupitia taasisi ya” Lyoto Foundation” alisema kuwa wanatarajia kuanza kutoa mikopo hiyo mwezi Julai Mwaka huu ili kuwasaidia Wananchi wa kata hiyo wanaotaka kufanya ujasiliamari kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.Mwisho