Na Grace Gurisha,TimesMajira Online
WAKAZI sita wa Kijiji cha Mpeta, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wamemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa awasaidie walipwe fedha zao sh.milioni 15, ambazo ni gharama walizotumia kuleta amani katika kijiji hicho kutoka na mapigano ya askari na wananchi yaliyotokea Oktoba 16 na 17,2015.
Pia, walifanikisha kupatikana kwa silaha mbili za Jeshi la Polisi (bastola na SMG) ambazo zilipotea katika mapigano hayo.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Gerald Ibrahim maarufu Serikali ambae ni mwakilishi wa wanakijiji hao na ndiye aliyeongoza kupatikana kwa silaha hiyo na kupatikana kwa amani kijijini hapo.
Amesema, baada ya tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma walikaa kikao ndipo Katibu Tarafa wa Nguruka alimweleza kuwa, amepata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa yeye unaweza kusaidia kupatikana kwa hizo silaha, kuzuia ghasia na kuleta amani.
“Nilikubali kufanya kazi hiyo iliyokuwa inagharimu sh.milioni 15 ambayo sijalipwa chochote hadi leo, kazi ilifanyika kubwa nilitawanya vikosi vya vurugu na kufanikiwa kupata silaha zilizopotea.
“Tunamuomba Waziri Mkuu atusaidie tulipwe fedha zetu kwa sababu, tulitumia gharama zetu kufanikisha kuleta amani na kupatikana kwa silaha,”amesema Ibrahim.
More Stories
Mpogolo amahukuru Dkt Samia
PPRA yatakiwa kuwa mfano kusimamia uadilifu Serikalini
Kamati ya Kudumu ya Bunge yaridhishwa ujenzi soko la Kariakoo