May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanahabari wazidi kujitosa ubunge na udiwani

Na David John, timesmajira,online

MWANAHABARI ambaye pia ni Mhariri wa Magazeti ya Kampuni ya New- Habari 2006
,Bakari Kimwanga leo amechukuwa fomu ya kugombea Udiwani kata ya Makurumla Manispaa ya Kinondoni.


Akizungumza Mara baada ya kuchukuwa fomu amesema kuwa anakipongeza na kukishukuru Chama chake kuweka mfumo wa wazi wa uchukuaji fomu.

Mhariri wa Magazeti ya kampuni ya New Habari 2006 Bakari Kimwanga akikabidhiwa fomu ya kuwania kugombea Udiwani kata la Makurumla wilayani Kinondoni leo kulia ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Sarama Mlaponi Leo Jijini Dar es salaam picha na David John .

Katibu wa Kata hiyo, Sarama Mlaponi amesema mchakato wa uchukuaji wa fomundani ya Kata hiyo mpaka leo huu takribani wanachama zaidi ya kumi wamejitokeza kuchukua fomu za udiwani.

Amesema mwamko upo japo sio mkubwa kwani hadi Jana walikuwa watatu lakini kufika leo idadi inaongezeka na sasa wamefikia zaidi ya kumi na kwamba upande wa wanawake ni mwanamke mmoja ambaye amejitokeza.

Wakati huohuo Mwandishi Mkongwe kutoka vyombo vinavyomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Angella Akilimali amechukuwa fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania ubunge wa Jimbo la Ukonga Jijini Dar es Salaam .

Angella amechukuwa fomu hiyo leo julai 15 katika Ofisi za CCM wilaya ya ilala Jijini hapa ambapo amesema amejipima ,amejitafakari nakuona anafaa kuchukua fomu.

Hata hivyo amefafanua kuwa kwamujibu wa Chama Chao kimetoa ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu ,hivyo huu si wakati wa kuzungumza chochote bali wakati utakapofika nakupata ridhaa kutoka kwenye Chama chake atakuwa na chakueleza.

Mwanahabari mkongwe kutoka vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi CCM Angella Akilimali akionyesha fomu za kugombea ubunge Jimbo la Ukonga mbele ya waandishi wa Habari hawapo pichani .Mara baada kuchukuwa katika Ofisi za wilaya ya ilala leo.

“Chama kimetoa ratiba ya uchukuaji na urejeshaji fomu kwamba mwisho julai 17 mwaka hivyo anakwenda kuijaza na Kisha kuirejesha kwa wakati ili kuacha Kura ya maoni itaamua na nani atapeperusha bendera ya Chama .”amesema angella