Na Mwandishi wetu Timesmajira,Online
BARAZA la Taifa Elimu ya Ufundi (NACTE), limetoa wito kwa Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vya Elimu ya Ufundi kuomba katika Vyuo vilivyosajiliwa na NACTE ili kupata uhakika wa elimu bora.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uthibiti, Ufuatiliaji na Tathmini NACTE, Geofrey Oleke katika ufungaji wa maonesho ya 16 ya vyuo vikuu Sayansi na Teknolojia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
” Nitoe wito kwa Wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Elimu ya Ufundi waombe katika Vyuo vilivyosajiliwa na NACTE ili wasije wakakosa nafasi, pia wazingatie machaguo ambayo yanaendana na matokeo yao ili kukidhi vigezo vya kudahiliw,”amesema
Ametoa rai kwa Wazazi kuwasaidia watoto wao kuhakikisha wanachagua vyuo ambavyo vinatoa Elimu kulingana na sifa za mwanafuzi na kusajiliwa na Baraza la Taifa Elimu ya Ufundi ‘NACTE’.
Â
Kwa upande wake Afisa Udahili NACTE, Levina Lunyungu amesema Baraza hilo lina mchango mkubwa katika Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda kwani wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuandaa wataalamu ambao wamekuwa wakihudumu katika nafasi Mbalimbali za kujenga uchumi wa nchi.
” Mchango wa NACTE kwenye Maendeleo ya Viwanda ni mkubwa sana kwani tumekuwa tukiandaa wataalamu katika sekta mbalimbali ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa ubobezi mkubwa” amesema LevinaÂ
Aidha NACTE imewakumbusha Wanafunzi waliochaguliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ambao walitakiwa kudhibitisha kupitia mfumo wa NACTE , imesogeza mbele mpaka Agosti 8,2021 ili kuwana nafasi ya kukamilisha mchakato huku akisisitiza kwa ambae hatothibitisha atakosa nafasi ya kujiunga na Chuo husika
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti