Na Penina Malundo,timesmajira,Online
JUMUIYA ya Wanafunzi wa Buguruni Viziwi (BUGURUNI VIZIWI ALUMN),imeiomba serikali na wadau mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi na kusaidia changamoto wanazokabiliana nazo.
Miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na kutokuwa na Ofisi ya kufanyia shughuli zao pamoja na miundombinu mbalimbali ya kuwawezesha katika kazi zao.
Akizungumza hayo hivi karibuni mkoani Dar es Salaam,wakati wa maadhimisho ya wiki ya Viziwi Duniani, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo,Subira Upurute amesema kundi la Viziwi ni miongoni mwa kundi ambalo linasahaulika na jamii yake kuona kama hawana haki sawa na wengine.
Amesema wamekuwa wakijitahidi kushirikiana na wadogo zao wanasoma shule hiyo kufanya matukio mbalimbali ili jamii ielewe kwamba ulemavu wao sio kushindwa.
“Katika Kuadhimisha siku wiki ya maadhimisho ya viziwi,tuliamua kukutana na wadogo zetu wanasoma shule ya Buguruni viziwi na kufanya usafi kwa lengo la utunzaji wa mazingira,”amesema Upurute
Amesema mbali na kufanya usafi huo pia waliweza kujadili hatima ya Shule yao ikiwemo kutatua changamoto zinazowatatiza ikiwemo kuchangiana ili kufanikisha ujenzi wa Karo la kufulia nguo.
“Huu ni mwaka wa nne tangu tuanze Jumuiya yetu ya Buguruni viziwi Alumn na kuhakikisha tunatatua changamoto zinazotukabili ili wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wasikumbane nazo,”amesema
Upurute amesema Jumuiya yao pia inakabiliwa na Changamoto mbalimbali kama ikiwemo ofisi, vitendea kazi hatuna na kuwapatia wanachama elimu ya ushirikishwaji katika mambo mbalimbali ya kijamii.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Chama cha kuhudumia Viziwi Tanzania(TSD) Yasini Mawe amewapongeza UMOJA wanafunzi hao kwa kujitoeza na kuwakumbuka wadogo zao katika shule hiyo.
Amesema umoja huo ulianzishwa mwaka 2015 katika shule chini ya Chama chao na kuwaunganisha wanafunzi wote waliosoma katika shule hiyo.
Naye Mmoja wa Wanafunzi hao,Joseph Hiza alisema huo ni mwanzo kwao na wanatarajia kufanya mambo mengi katika shule hiyo kwa lengo la kuonyesha ushirikiano kwa wanafunzi wenzake.
Mwishooo
ReplyReply allForward |
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakani
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best