May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi 30 wahitimu mafunzo ya ndege nyuki

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

MKUU wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Aristid Kanje amewapongeza wahihitimu 30 wa mafunzo ya urushaji wa ndege nyuki wa awamu ya kumi na nne ambao wataenda kusaidia utendaji kazi wa kurusha ndege ili kuhakikisha usalama wa anga na vyombo virukavyo angani.

Ameyasema hayo Novemba 08, 2023 Jijini Dar es Salaam MKUU wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Aristid Kanje wakati wa hafla fupi ya kuwaaga na kuwapatia vyeti wa wahitimu 30 ambao wamemaliza mafunzo yao ya wiki mbili ambayo yalianza Novemba 14, 2023 katika Chuo cha Csafiri wa Anga.

Kanje amesema wanafunzi wengine waendelea kutumia fursa hiyo ya mafunzo ambayo yanatija na gharama rafiki kwa watanzania, jambo ambalo limepelekea kuwavutia wanafunzi mbalimbali kutoka ukanda huu wa nchi za Afrika Mashariki “hapa wako wanafunzi wa kenya na Ugamda pia”

“kuna kipindi hapa walikuja watu kutoka marekani na wakatoa mafunzo haya ya urushaji drone ambapo gharama zake zilikuwa shilingi milioni 6 kwa wiki mbili na hayakuwa mafumzo ya vitendo, lakini sisi tunataka watu wajue sheria, wapate maarifa ya kutosha ili wawe na uwezo wa kutosha” Mkuu wa Chuo Aristid Kanje

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi muhitimu Lightness Massawe amesema mafunzo hayo yameongeza ujuzi na umakini katika uendeshaji wa ndege wa nyuki, pia wamepata fursa ya kukutana na watu mbalimbali jambo ambalo limepelekea kubalishana mawzo na ujuzi.

Aidha, mafunzo ya ndege nyuki yametufunza kuyafikia maeneo hatarishi kwa bianadamu na kufanyiwa kazi na ndege nyuki, maeneo hayo mi kama majanga ya moto na mafuriko.

Hivyo, licha ya mafunzo hayo kumekuwa na changamoto ya vitendea kazi kwa vitendo kuwa vichache na kutokuendana na idadi ya wanafunzi, pia taaluma hiyo imekuwa ikivamiwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya kazi bila kuwa na ujuzi wa viwango kilingana na ithibati za kimataifa.