January 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wana CCM Chanika watakiwa kufanya kazi kujenga Chama

Na Heri Shaaban (Ilala )

Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Chanika Wilayani Ilala kimewataka viongozi wa chama hicho kufanya kazi za chama kwa ajili ya kujenga chama badala yake wasitengeze makundi na kuleta nongwa ndani ya chama .

Mwenyekiti wa CCM Chanika William Mwilla, alisema hayo jana wakati wa ziara yake ya Utekelezaji wa ahadi zake kukabidhi matofali,saruji na Vyoo katika matawi ya ccm Yongwe na Kidugalo ambayo miaka yote matawi hayo yalikuwa hayana vyoo.

“Viongozi wangu wa matawi Kata ya chanika sasa tunaelekea katika chaguzi za Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 wa Rais wabunge na madiwani Sasa tujipange kuwa wamoja kusaka Dola chanika ni ngome ya CCM kila kiongozi asimamie Majukumu yake ya chama na Jumuiya tuache kutengezeana Nongwa na makundi ndani ya chama hayana Afya kichama ” alisema Mwilla

Mwenyekiti Mwilla aliwataka Viongozi wa chama Chanika kuwa wamoja kila mmoja kusimamia Majukumu yake katika kujenga chama na kuakikisha chama cha Mapinduzi CCM kinashika Dola chaguzi zake zote .

Alisema CCM Chanika itaendelea kushika dola Diwani wao kwa Sasa Ojambi Masaburi na Mbunge wa Ukonga Jery Silaa, wapewe Ushirikiano kwa pamoja wanatekeleza Ilani vizuri na kusimamia miradi ya Maendeleo ya Kata na Jimbo la Ukonga .

Akizungumzia Utekelezaji wake wa ahadi katika chama alisema wakati anagombea uongozi wa chama Kata ya chanika alitoa ahadi ya kujenga vyoo katika Ofisi za chama katika matawi ya chanika sasa ameanza kutimiza ahadi yake sehemu ya utekekezaji wa Ilani ya Chama .

Mwenyekiti Mwilla aliwataka Viongozi wa CCM Yongwe na Kidugalo wasimamie ujenzi wa vyoo vya matawi ya chama sasa limebaki jukumu lao la ujenzi wakiimaliza ujenzi viongozi wa chama watakuja kuzindua .

Katika hatua nyingine aliwataka wafanye Siasa na uchumi Katika maeneo ya viwanja vya chama wajenge fremu za Biashara na kuwakodisha Wafanyabiashara kwa mkataba .

Alitumia nafasi hiyo kumpongeza Katibu wa chama cha Mapinduzi aliyemaliza muda wake Tatu Mpemba, kwa kujenga Ofisi ya chama ambaye inatumika hivi sasa kwa ajili ya Shughuli za chama cha Mapinduzi .

Katibu wa Siasa na Uenezi wa kata ya chanika
Jafari Kwembe akimpongeza Mwenyekiti wa CCM wa kata William Mwilla wa kutimiza ahadi yake ndani ya chama cha Mapinduzi .

Mwenezi Jafari Kwembe alimtakia Afya njema Mwenyekiti wa CCM William Mwilla aweze kufanya kazi za chama vizuri na kutimiza malengo yake

Mwenezi Jafari aliwataka Wana CCM chanika kuwa wamoja katika kujenga chama na Serikali katika kuelekea katika chaguzi za kushika Dola .