Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Serikali imewataka wafungwa watakaomaliza kutumikia vifungo vyao gerezani kutumia ujuzi waliopata kujitengenezea kipato ili kuepuka kujiingiza tena katika uhalifu.
Maagizo hayo yametolewa Novemba 20, 2023 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini wakati alipokuwa akihitimisha ziara yake ya Kikazi katika Gereza la Mahabusu Mugumu Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
“Dhamira ya Serikali ya ni kuona watu wake wakipanda kiuchumi ndio maana hapa gerezani sio sehemu ya mateso bali ni sehemu ya mafunzo na tunawapa mafunzo wafungwa ili wakitoka watumie ujuzi huo kujitengenezea kipato,”amesema Sagini.
Pia Sagini amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufyatuaji tofali, ushonaji,uashi,uchomeleaji vyuma, uselemala,ufugaji ambayo imechochea wafungwa kuwa na ujuzi ambao utawasaidia huko uraini.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu