May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Biteko akagua majengo Wizara ya Nishati, Sera, Uratibu na Bunge

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko leo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Nishati na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali- Mtumba jijini Dodoma.

Dkt.Biteko katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jimmy Yonaz, na watendaji mbalimbali kutoka Wizara hizo mbili.

Katika Jengo la Wizara ya Nishati, Dkt. Biteko alikuta ujenzi unaendelea ambao kwa sasa umefikia asilimia 69 ambapo Mkandarasi ni
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Aidha, ujenzi wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu), unaendelea vizuri huku ukiwa umefikia asilimia 74 na
Mkandarasi ni SUMA JKT.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt.Doto Biteko (wa Tatu kulia) akikagua jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma. Pamoja naye ni Katibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt.Jimmy Yonaz (wa kwanza kushoto) pamoja na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).