December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wafugaji washauriwa kufuga kisasa

Na Esther Macha,timesmajira,online,Mbeya

WAFUGAJI nchini wameshauriwa kufuga aina za kisasa za ng’ombe kwa madai kuwa licha ya kuongeza tija ya uzalishaji wa maziwa lakini pia zina himili hali ya hewa kulingana na eneo husika.

Ushauri huo umetolewa na Meneja wa kampuni ya Highlands Ranches Limited (Usangu Ranch)Yakub Shiran wakati akizungumza na gazeti hili kwenye maonesho ya wakulima Nanenane yanayofanyika Kikanda mkoani mbeya .

Shiran amesema ni wakati sasa wafugaji wakaacha na ufugaji wa ng’ombe usiokuwa na tija na badala yake waangalie aina za mifugo hiyo ambayo itamnufaisha kwa kuhakikisha anajiongezea kipato.

Amesema kuwa ng,ombe wa nyama hata ufugaji wake hauna grama kwa mfugaji na pia hata magonjwa ya mifugo kwa aina ya ng,ombe hao wana uvumilivu .

Hata hivyo Shiran alisema ufugaji wa ng,ombe wa nyama ni muda mfupi na kwamba ufugaji bora ni huu na kwamba kwa bonde la usangu mifugo inahimili magonjwa.

“Ng,ombe hawa wanahimili hali ya hewa ya sehemu yeyote ile hivyo ni rahisi kuwafuga”amesema