Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha
Wafanyabiashara mkoani Arusha wameaswa kuhakikisha kuwa wanakuwa wazalendo Kwa kutumia mashine za kielektroniki(Efd) hasa wanaponunua au kuuuza bidhaa Kwa wateja wao
Endapo kama wafanyabiashara watakuwa waadilifu basi watakuwa wamechangia kuinua pato la Taifa ambalo linategemea zaidi Kodi
Hayo yameelezwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela siku chache zilizopita wakati akizindua kampeni ya tuwajibike ambayo ilizinduliwa na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)mkoa wa Arusha
Mongela alisema kuwa suala la utoaji wa risiti ni suala ambalo linatakiwa kutekelezwa na mfanyabiashara yoyote Yule ambaye anatoa huduma Kwa wateja wake
“Wapo baadhi ya wafanyabiashara ambao sio waaminifu ambao mara nyingi huwa wanashindwa kutekeleza lengo la mashine hizo Mimi niwaambie kuwa hawafanyi vizuri na wanavunja sheria za nchi na kwa saaa wanatakiwa kujua kuwa Kodi ndio chanzo cha maendeleo ya nchi”aliongeza Mongela
Katika hatua nyingine Mongela aliitaka TRA mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa kampeni ya tuwajibike haibaki Arusha Jiji pekee Bali elimu hiyo iweze kusambaa Hadi kwenye ngazi za wilaya zote za mkoa wa Arusha
Naye Meneja wa TRA mkoa wa Arusha Bi Eva Raphael alisema kuwa pamoja na kuwa wamezindua kampeni hiyo lakini wao kama mamlaka watahakikiaha kuwa wanafanya KAZI kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi
Eva alisema kuwa kampeni hiyo itaweza kuwafikia wafanyabiashara wote wa mkoa wa Arusha
Aliwataka wafanyabiashara kuanzia SASA kuhakikisha pia wanatoa risiti ambazo ni sahihi kwa wateja wao nakuachana na tabia ya kutoa risiti ambazo haziendani na bei halisi.
More Stories
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi
Rais Samia apongezwa kwa miongozo madhubuti ya ukusanyaji wa kodi
Mwenda:Siku ya shukrani kwa mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua,kuwashukuru