Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
WADAU mbalimbali Jijini Mbeya wameombwa kushirikiana katika kutengeneza mifumo salama ya utoaji taarifa na upatikanaji wa masuala ya watoto wenye uhitaji na wasio na uhitaji ili waweze kutoa taarifa bila ya hofu kwa kuwa wanaweza kukutwa na baya lolote pindi watakapotoa taarifa ya kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa idara ya Miradi wa Child Support Tanzania (CST)inayojishughulisha na elimu Jumuishi watoto wenye ulemavu Hildergade Merhab wakati wa kikao cha kamati ya miradi ya shirika hilo ambacho kilikuwa kikijadili kazi miradi ambayo imetekelezwa kwa mwaka mmoja uliopita pamoja na miradi mipya walinayo katika Taasisi hiyo.
Aidha Merhad amesema kuwa kikao hicho pia kiliangalia masuala ya ulinzi na usalama kwa watoto lakini pia wajibu wa kamati ya miradi ambayo wamo walimu,wakuu wa shule,waandishi wa habari,maafisa ustawi wa jamii,wataratibu elimu kata pamoja wanafunzi wenye mahitaji maalum na wasio na mahitaji,dawati la jinsia(Polisi)na katika suala la ulinzi wa watoto kila mmoja ana nafasi yake katika kuhakikisha kunakuwa na ulinzi kuwa suala la ulinzi jumuishi kwa watoto wenye ulemavu.
“Kama Child Support Tanzania tunaomba sana wadau wetu kwa nafasi zao kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha kutengeneza mifumo salama ya utoaji taarifa na upatikanaji ili kila mmoja wetu hasa watoto wetu wenye mahitaji na wasio na mahitaji wanaweza kutoa taarifa bila kuwana hofu kuwa kunabaya linaweza kumkuta,lakini hata wale wanaotoa taarifa waweze kulindwa na wanaopokea taarifa kwa kushirikianana serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na jeshi la polisi kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa kwa watoto waliofanyiwa vitendo vya ukatili pamoja na idara ya afya kupitia hospitali ya Rufaa ya Kanda yaMbeya kukaa na watoto hawa”amesema Mkuu huyo wa Miradi.
“Kwa mwaka huu tumepata miradi mitatu mipya miradi ambayo inaenda kufanywa Rukwa, Katavi na Songwe ambao unafadhiliwa na serikali ya Ujerumani kupitia cbm lakini pia tuna mradi wa maktaba Jumuishi ambao ni mwendelezo wa miradi ya maktaba ambayo ipo mkoa wa Mbeya inayooenda kufanywa shule ya msingi Katumba (2) shule ya msingi Mbalizi (1) pamoja na Itiji huu ni mwendelezo wa mradi wa mazoezi tiba ambao unaendelezwa katika shule ya Jumuishi ya Child Support Tanzania ambapo tunaenda kuangazia masuala ya mazoezi tiba kwa watoto wenye mahitaji maalum”amesema .
Damas Mwambije ni Mwenyekiti wa kamati za miradi ya Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Child Support Tanzania (CST)amesema kuwa kikao hicho hufanyika kila baada ya miezi sita ambapo kamati hiyo husimama katikati ya wanufaika wamradi na watoa mradi wenyewe ambao ni CST na kamati husimama kwa ajili ya kuangalia kilichoandikwa kama kimetekelezwa na kuwa mpaka sasa jumla miradi miwili mikubwa ikiwemo mradi wa peleka rafiki rafiki zangu shule ambao unaendelea katika mkoa wa Mbeya ,mradi mwingine unaenda kuanza kwa mikoa ya Rukwa ,Songwe na Katavi mradi wa uhusishaji wa rasilimali kwa ajili ya Elimu jumuishi.
“Lakini huu wa peleka marafiki zangu shule ni mradi utakaohusisha upimaji kielimu ,afya na afya stahiki ambazo zinapaswa watoto wenye ulemavu na watoto kwa ujumla wake waweze kuzipata ili waweze kuwa vizuri katika masomo yao na kuleta maendeleo katika nchi yao “amesema.
Mwakilishi wa Walimu wakuu katika mradi wa Child Support Tanzania ambaye ni mkuu wa shule ya msingi Kyela , Asheri Ayoub amesema kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikiwafikia watoto wengi katika upimaji watoto wenye ulemavu na ukarabati na ukarabati wa miundombinu ya watoto wenye ulemavu shule ya msingi Kyela.
“Tumelenga kuwafikia watoto wengi zaidi na Mei 31 ,2024 tutakuwa na mkutano mkubwa shule ya msingi Kyela ambao utalenga wazazi wote kwa ajili ya utambuzi wa watoto wenye mahitaji maalum hili litakuwa jambo kubwa na kipekee na itasaidia jamii kuelewa maana ya elimu jumuishi “amesema.
More Stories
TAKUKURU,rafiki yanufaisha wananchi Mwanza
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa