May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wadau wa kilimo hai waendelea kuhamasisha matumizi ya mbegu asili

Na David John, Timesmajira online, Mbeya

MRATIBU wa Mtandao na utunzaji wa Bioanuai Tanzania Abdallah Mkindi amesema kuwa wapo katika maonyesho ya nanenane wakiongozwa na kauli mbiu ya mchango wa mbegu za asili katika kufikia asili 10 ya uzalishaji mazao na wao kama wadau wa kilimo hai ili kufikia ajenda ya serikali ya kufikia mwaka 2030 kilimo kiwe kimekuwa kwa asilimia hiyo hivyo wadau wa kilimo hai ambao wamejikita kwenye mbegu za asili hiyo nifursa muhimu sana kwao.

Amesema kuwa wao kwa lengo la kuhamisha matumizi ya mbegu za asili pamoja na mbinu za kilimo hai ili kufikia hiyo ajenda ya serikali kwenye banda lao kuna mbegu zaidi ya aina 50 ambazo zinatumika na wakulima na nyingi zimetoka katika wilaya ya karatu na zingine zimetoka Morogoro, Mbeya , Songwe pamoja na Dodoma.

Abdallah ameyabainisha haya Agosti 4 jijini Mbeya katika maonyesho ya nanenane yanayoendelea mkoani hapa ambapo amesema wadau wa kilimo hai wapo kwa ajili ya kuonyesha mbegu hizo ambazo pia zinatumika na wakulima hivyo imani yake nikuona zinapotumika vizuri ikiwa pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu ili tija ionekane na inapofika 2030 kilimo hicho kiwe kimekuwa kwa asilimia 10 kama ajenda ya serikali inavyosema.

“Kimsingi mbegu za asili ni muhimu sana katika kilimo chetu ,lakini vilevile pembejeo zingine za kilimo hai kama viwatilifu, mbolea ambavyo vyote vipo kwenye banda letu hizi pembejeo ambazo zinatumika katika uzalishaji ili hatimaye kuweza kuzalisha chakula salama na afya ya binadamu na pia katika utunzaji wa mazingira hivyo watu wajitokeze katika banda letu kuona aina mbalimbali za mbegu na kuweza kununua ili waweze kuzitumia.”amesema

Tupo hapa hadi mwisho wa maonyesho haya imani yetu kwa siku zilizobaki tuweze kutembelea mabanda mengine ili kujifuza wanacho kifanya ili wakatiu mwingine tunapokuja tuweze kujua ni enep gani tunahitaji kuboresha.”amesisitiza Mratibu Abdallah

Kwa upande wake mdau wa kilimo hai kutoka Mtandao wa kilimo Deodatus Athony Mtaalamu kutoka katika maeneo ya mkoa wa Singida wilaya ya Manyoni amesema yeye ni mkulima ambaye ameamua kujifunza katika maonyesho hayo hususani kupitia banda la kilimo hai lililopo katika viwanja vya maonyesho ya nanenane jijini mbeya.

Amefafanua kuwa yeye amejifunza mambo mengi sana katika banda la kilimo hai kwani amejifunza upatikanaji wa mbegu bora za kilimo hai upatinaji wa dawa za asili lakini baada ya kuyzunguka amejifunza mambo mengi sana,ameona mbegu nyingi za kilimo,mbolea za asili.

“Nawakaribisha wakulima wenzangu kwenye banda la kilimo hai ili kuweza kujifunza kwani kuna vitu vingi sana kuna asali kuna mafuta ya alizeti ambayo hayana kemikali yeyote hivyo nawakaribisha sana kujionea ninyi wenyewe.”Amesema Athony