Angela Mazula, Timesmajira Online
Ni Bunge la 12 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo hivi sasa linaendelea katika shughuli zake za kibunge za upigaji wa kura za kuchagua Spik awa bunge hilo.
Mwenyekiti wa muda William Lukuvi ndio msimamizi wa zoezi hilo kwasasa hapo bungeni Dodoma ambapo mpaka sasa Spika wa bunge lililopita ndio mgombea pekee ambaye amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo
Job Ndugai ambaye ameshinda nafasi ya ubunge katika jimbo la kongwa kutoka katika mkoa wa Dodoma kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) ndiye mgombea pekee wa kiti hicho.
Aidha wakati huo huo Aida Kenani Mbunge wa Nkasi kaskazini wa tiketi ya chama cha Democrasia na maendeleo (Chadema) alitaka kujua ni nini kipya atafanya kwa kupitia nafasi hiyo ambayo anagombea, akijibu swali hilo Job Ndugai amesema atahakikisha kuwa bunge hilo la sasa linaenda vizuri na kuhakikishia kuwa hakuna tofauti zitakaojitokeza katika utekelezaji wake katika wa kiti hicho cha Spika.
Ni jumla ya wabunge 263 ambao wanapiga  kura za kumchagua Spika wa bunge hilo.
More Stories
CP.Wakulyamba ashuka Katavi na Nguzo nne za Uongozi
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Maandalizi ya mkutano mkuu CCM yapamba moto