January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waandishi watakiwa kuendelea kutoa uzito habari za Uviko 19

Na Martha Fatael, Dar es salaam

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuendelea kuzipa uzito taarifa sahihi za kitaalamu na ufuatiliaji wa karibu juu ya athari za Uviko 19 ili kuielimisha jamii ichukue tahadhari na kupata Chanjo ya ugonjwa huo.

Kadhalika wanahabari wametakiwa kuandika habari za kiutafiti kuhusu ugonjwa huo kwani bado wataalam wanaendelea kutoa ripoti mbalimbali ambazo jamii inapaswa kujulishwa kinachobainika.

Hayo yamesemwa wakati wa warsha kwa wanahabari wa nchi zaidi ya 35 kutoka Tanzania na Katibu wa jumuiya ya wanahabari katika nchi za Kiafrika (CAJ), William Oloo ambapo amesema taarifa za uwepo wa ugonjwa wa Uviko 19 mwanzoni mwa mwaka 2020 ulisababisha janga la kidunia.

Amesema janga Hilo liliathiri mfumo wa maisha na kusababisha na njia sahihi za utolewaji wa taarifa hususani kuhusu ugonjwa wa Uviko 19.

Amesema ni jukumu la wanahabari kuhakikisha taarifa sahihi zinaifikia jamii ili kukabiliana na janga lililopo.

Oloo amesema CAJ kwa kushirikiana na Chama Cha wanahabari Nchini Kenya (KCA), pamoja na Article 19 imebaini mradi kuongeza ufanisi wa kukabiliana na Uviko 19 kwa nchi za Kiafrika na kwamba mpango huo na kuhusisha nchi za Kenya, Tanzania na Ethiopia.

Amesema lengo ni la mradi ni kusaidia ishawishi na uhamasishaji baina ya asasi za kiraia, vyombo vya Habari katika kuhakikisha sheria,sera na taratibu za utoaji wa taarifa sahihi Uviko 19 zinazingatiwa.

Amesema kwa kufanya hivyo kutapunguza wingi wa habari potofu kuhusiana na athari na maambukizi ya ugonjwa wa Uviko 19.

Mapema, Meneja wa program kutoka shirika la ARTICLE 19, Sarah Wesonga amesema uwepo wa taarifa zisizosahihi umesababisha jamii kutoamini taarifa zinazotolewa kuhusiana na kupunguza maambukizi katika jamii.

Amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa na serikali katika kuelimisha jamii na hatua zinazopaswa kuchukuliwa na wananchi katika kujikinga na umuhimu wa kupata chanjo.

Amesema uwepo wa taarifa potofu imekuwa ukilenga mkanganyiko katika jamii na utata ama wananchi wapate chanjo ama laa jambo ambalo linasababisha athari kuongezeka.

Wesonga amesema kumekuwepo na taarifa nyingi katika mitandao ya kijamii na vyanzo vingine vya taarifa katika kueleza utolewaji wa Chanjo na hivyo kuipotisha jamii.

Mapema Katibu mkuu wa Chama Cha wafanyakazi wanahabari nchini (Jowuta) Seleman Msuya amesema warsha hiyo umekuja wakati muafaka na.kugusa majukumu ya wanahabari siku hadi siku kuhusiana na athari za Uviko 19.

Amesema wanahabari kama ilivyo katika nchi nyingine wanapata changamoto katika kuandika athari za ugonjwa huo ikihusisha masuala ya sera na upashanaji habari ambayo imekuwa na vikwazo kadhaa.

Msuya amesema wanahabari kama binadamu wengine nao wameathirika na ugonjwa huo huku baadhi wakipoteza maisha.

Amesema ni jukumu la wanahabari in kuhakikisha watanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla wanakuwa salama dhidi ya Uviko 19.

Meneja wa Portfolio wa mradi wa COVID 19 Response in Africa, Together for Reliable information (ARTICLE 19) Moses Opiyo akizungumza wakati wa warsha kwa wanahabari wa nchi zaidi ya 35 kutoka Tanzania iliyofanyika jijini Dar es salaam

Huyu ni katibu mkuu wa chama Cha wafanyakazi wanahabari Tanzania(JOWUTA), Seleman Msuya akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya wanahabari Tanzania iliyofanyika jijini Dar es salaam