May 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Gwajima aviasa vyuo vya afya, ahimiza maadili

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima amewataka wamiliki wa vyuo vya Afya vinavyomilikiwa na Sekta Binasi hapa nchini kuwaandaa wataalamu wa kada za afya watakapo ajiliwa wafanye kazi kwa kuzingatia maadili,Uzalendo,Unyenyekevu na utii wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa.

Dkt Gwajima ametoa agizo hilo leo 27.11.2021 katika mahafali ya kwanza ya Chuo cha Afya Mt.Maximilliancolbe cha mjini Tabora ambacho ni miongoni mwa vyuo 192 vya Afya vilivyosajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ( NACTE ).

Amesema kuwa serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Sekta binafsi kukuza uchumi wa Taifa hivyo wamiliki wa vyuo wanawajibu mkubwa wa kusimamia nidhamu ya wanafunzi ili Taifa lipate watumishi waadilifu watakao kwenda kutoa huduma bora kwa jamii ambayo inategemea wataalam kuokoa maisha ya watu pindi wanapougua magonjwa mbalimbali.

Aidha Dkt Gwajima amewataka vijana kufanya kazi kwa kuzingatia maadili kwa weledi ili kupunguza malalamiko kwa jamii kwani kutoa huduma bora kwa mgonjwa ni faraja wakati wa kupatiwa matibabu

Pia amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupatiwa chanjo kwa kuwa serikali imepata chanjo nyingi kwa ajili ya kuwakinga wananchi ili ku tvwaepusha madhara makubwa kwa jamii hasa kwa wakati huu unaotajwa kuibuka kwa wimbi jipya la uviko 19 la nne.

Katika mahafari hayo,Dkt Gwajima amewatunuku Stashahada ya sayansi ya Famasi kwa wahitimu 37 katika Chuo cha afya Mt.Maximiliancolbe cha mjini Tabora