Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
WAANDISHI wa Habari mkoani hapa wamehimizwa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF),ili kuwa na uhakika na matibabu endapo watapatwa na maradhi.
Wito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC),Edwin Soko, wakati wa hafla ya ugawaji wa kadi ya bima ya afya kwa wanachama 16 wa klabu hiyo waliojitokeza kujiunga na mfuko huo pamoja na kadi za uanachama wa MPC kwa wanachama 10,iliyofanyika Jijini Mwanza.
Soko amesema,waandishi wa habari ni muhimili wa nne,hivyo wanapokuwa na afya njema au wanapougua na kukuwa na uhakika wa kupata matibabu wafanyakazi zao vizuri na taifa kuendelea kupata habari mbalimbali.
Pia amesema,wamiliki wa vyombo vya habari wawasaidie waandishi wao kupata bima za afya ili waweze kufanya kazi katika mazingira salama na yenye uhakika wa matibabu endapo atakubwa na maradhi kwani afya ndio msingi.
Akizungumzia wakati wa akifungua hafla hiyo Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk and Chair Foundation Alhaji Sibtain Maghjee amewapongeza waandishi wa habari kwa kutambua umuhimu wa kadi hizo.
Aliongeza kuwa kadi hizo zitawasaidia kuhakikisha wanakua salama na wenye afya njema katika shughuli zao za kila siku kwani inasaidia kupunguza gharama maana taasisi kabla ya kuwakatia bima wagonjwa wanaowasaidia ilikuwa inatumia fedha nyingi katika matibabu lakini sasa wanatumia gharama ndogo.
Katika hatua nyingine,Alhaji Maghjee amechangia mfuko wa kijamii wa waandishi wa kusaidiana kiasi shilingi laki tatu (300,000).
More Stories
Madaktari wa Tanzania, Comoro waanza kambi kwa kishindo
Watakiwa kushirikiana kutikomeza matatizo ya lishe
CCBRT yazidi kuunga mkono juhudi za Rais Samia