Na Penina Malundo.
KAMPUNI inayoshughulisha na Uchakataji wa Samaki ziwa Tanganyika (Alpha Tanganyika Flavour),imetoa wito kwa vijana wa mtaa wa mzimuni kujitokeza kwa wingi katika bonanza la mpira wa miguu linaloendesha na kampuni hiyo kwa lengo la kuunga mkono sekta ya michezo kwa serikali ya awamu ya sita.
Akizungumza hayo juzi,Mkurugenzi wa Kampuni hiyo,Alpha Nondo wakati wa michuano ya bonanza la mpira huo katika viwanja vya shule ya msingi mzimuni,alisema kampuni yao imesapoti vijana wanaishi katika mtaa wa mzimuni ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kutimiza ndoto zao.
Amesema wapo vijana ambao wanatamani kufika mbali kupitia michezo hivyo kupitia bonanza hilo litaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo yao kwa kuamua kutumia bonanza hilo vizuri.
”Katika kurudisha shukrani kwa jamii kama kampuni ya Alpha Flavour Tanganyika tumeamua kusaidia kundi hili la vijana wa mzimuni kwa kuwaandalia bonanza hili ambalo mshindi wa kwanza ataweza kupata medari,kombe pamoja na fedha taslimu huku mshindi wa pili atapatiwa medari pekee yake,”amesema na kuongeza
”Pia kampuni hiyo imeweza kuwasapoti kwa kuwapatia jezi,mipira pamoja na viatu vya kuchezea wachezaji wote 50 huku tukiwataka vijana hao kuhakikisha wanatumia mazoezi kama sehemu ya kuwajenga kikamilifu katika kuwa na ushirikiano,”amesema.
Amesema kama kampuni inamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa wachakachaji wa samaki kupitia W izara yake ya Uvuvi kwa kuendelea kuwa karibu nao na kuhakikisha wanamazingira mazuri ya biashara.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Idrisa Kata ya Mzimuni, aliishukuru kampuni hiyo kwa kuwasaidia vijana hao,na kuwafanya wawe watu wa mazoezi na kuaacha kukaa vijiweni.
Amesema bonanza hilo limeweza kubadilisha maisha ya vijana hao na kufanya kila siku jioni vijana wanakuwa wanaenda katika viwanja hivyo na kufanya mazoezi tofauti na miaka ya nyuma.
”Tunashukuru kwa mdau kutusapoti na kutusaidia,kuwasaidia na kuwa kitu kimoja kwa kutumia michezo,Bonanza hili limewabeba vijana wengi kuacha kukaa vijiweni sasa wanakuja mazoezini na kufanya mazoezi,”amesema.
Naye Mfanyakazi wa Alpha Flavour Tanganiyika, Bakari Ally alisema kampuni yao imehamasisha vijana kupenda michezo kwani ni afya.”Michezo inaunganisha watu, kukutana na kuunganisha watu hivyo kampuni hii imekusanyika kwaajili ya michezo ya mipira ya miguu,tumeweka mashindano kwaajili ya kuisapoti serikali kama mama Samia alivyokuwa na spidi kila sekta,”amesema na kuongeza
”Tunamsapoti Mama Samia tumekuja kupambana ili kuweka hali ya michezo vizuri kwa vijana wa mtaani na hii inasaidia kukuza vipaji na kutimiza ndoto zao,tumeanza ila litakuwa linamuendelezo na kufanya mechi mbalimbali kwa watu,”amesema.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM