December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Uzinduzi wa mpango wa kugawa mbolea bure kwa wakulima katika picha

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akimkabidhi mbolea mmoja wa wakulima wa Kata ya Mlowo mkoani Songwe, Issa Ngoi
wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa kugawa mbolea bure kwa wakulima ujulikanao kama “Action Africa”. Zaidi ya tani 12,500 zenye thamani ya sh. bilioni 16.5 zitagawiwa kwa wakulima 83,000, nchi nzima.
Mpango huo umezinduliwa leo na Waziri Hasunga Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya YARA Tanzania, Winstone Odhiambo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali, Mstaafu Nicodemus Mwangela. Na Mpiga picha Wetu.