
Na Israel Mwaisaka, Nkasi
Mkuu wa shule ya sekondari Mkole wilayani Nkasi Hamisi Hussein amesifu uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika elimu kwa kujenga vyumba Bora vya madarasa,maabara,ajira nyingi za walimu ikiwa ni pamoja na vifaa vya kufundishia na kujifunzia
‎
‎Hayo ameyasema jana kwenye mahafali ya kidato cha nne, ambapo amedai kuwa sector ya elimu imeboreshwa kwa kiasi kikubwa na kuwa matokeo ya uwekezaji huo yameanza kuonekana kwa miaka kadhaa shule za wilaya ya Nkasi zimekuwa zikifanya vizuri katika mitihani ya kitaifa. Na kuongeza kuwa hata wanafunzi wake wa mkole wameendelea kujifunza kwa vitendo kutokana na maabara za kisasa
‎
‎Amesema kuwa mafanikio hayo hayaji kiurahisi bali yanatokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali na kuwataka Walimu kuongeza bidii na maarifa katika ufundishaji kama njia ya kuunga mkono jitihada hizo nzuri zinazofanywa na Serikali katika kuboresha mazingira Bora ya elimu Nchini.
‎
‎Wanafunzi katika risala Yao walimweleza mgeni rasimi kwamba licha ya mafanikio kadhaa yaliyopo katika shule hiyo pia wanazo changamoto kadhaa kama ya upungufu wa hostel kwa wasichana,upungufu wa maji,vitabu vya masomo ya Sanaa ikiwemo viti na meza kwa Wanafunzi na Walimu.
‎
‎Akijibu risala hiyo mgeni rasmi afisa rasilimali Watu wa Msipazi Farm Juma Ayoub alidai kuwa amezichukua changamoto zao na kuwa atazipeleka kwa mkurugenzi wa Msipazi Farm ili waweze kutafuta namna ya kuzikabili changamoto hizo .
‎
‎Amesema kuwa changamoto zilizopo ni nyingi lakini wataweza kushughulikia na changamoto zile watakazokuwa na uwezo nazo kwa Sasa.

More Stories
Jaji Mshibe asisitiza maandalizi ya Kisekta katika kukabiliana na athari za El Nino
Wki ya Elimu kuibu vipaji ,wabunifu
PPAA yawanoa wakandarasi mazingira ya haki zabuni