April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Utelekezaji watoto Mbarali unaofanywa na wanaume kukomeshwa

Na Esther Macha, Timesmajira,Online, Mbarali

ASILIMIA kubwa ya utelekezaji wa watoto katika halmashauri ya wilayaya Mbarali mkoani Mbeya unatokana na unyanyasi wa wanaume kwawanawake ambao hutokana na vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwavikiendelea kufanywa na kupelekea kutekeleza familia zao .

Wilaya ya Mbarali imekuja na mwarobaini wa changamoto hiyo ambapouongozi uongozi wa halmashauri hiyo umepanga kukabiliana na tatizohilo kwa kutembea kata , vitongoji ,vijiji kuangalia kiini chatatizo hilo na kupata suluhisho na tatizo hilo kuisha kabisa .

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mbarali mkoani Mbeya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Itamboleo, TwalibLubandamo wakati wa kikao cha mkutano wa kawaida wabaraza la madiwani wilayani humo uliofanyika jana katika ukumbi waMaji.

Lubandamo amesema kuwa kero kubwa ambayo anakutano nazo katika ofisiyake ni ugomvi wa ndoa na familia zilizotelekezwa na kusema mpakasasa analea familia sita zilizotelekezwa .

‘’Nina mtoto mwingine ambaye nimemchukua Igurusi Sekondari yupovizuri sana kimasomo ambaye amepata ufaulu mzuri sana kwenye matokeoyake ya kidato cha Nne ,ninao watoto wengi ninaolea sisi wanaumetumekuwa wanyanyasi wakubwa kwa wanawake hivyo wanawake wanaenda kupata shida na watoto kwa hiyo kero nyingi tulizo nazo asilimia kubwa ni wanawake kuja na familia zao na ugomvi wa ndoa unakuta mudamwingine mwanamke anakuja kapigwa mpaka katolewa sikio kung’atwa ulimi kwakweli wanaume tumekuwa wakatili sana ,wiki iliyopita alikuja Mamammoja na watoto sita hawajala chochote hivyo ilibidi kama halmashauritujichange kumsaidia mama huyu ‘’amesema Mwenyekiti huyo wahalmashauri .

Akizungumzia zaidi Mwenyekiti huyo amesema kama halmashauri wamejipanga kwa kukabiliana kuwa kila kijiji , kitongoji kuanziaMwezi marchi kwenda kuangalia changamoto za wanawake na kuhakikishazinakwisha moja kwa moja.

Kaimu Mganga mkuu Halmashauri ya wilaya ya Mbarali idara ya afya naustawi wa jamii na lishe , Dkt.Ray salandi amesema kuwa kitengo chaustawi wa jamii kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha walikuwa na jumlaya migogoro ya kifamilia 334 ambapo kwa asilimia kubwa migogoro hiyo imetokana na ukatili wa kimwili kwa maana ya vipigo ambavyovinafanya jumla ya vipigo 113 ambayo ni sawa na asilimia 34iliyosuruhishwa kwa kipindi cha robo ya pili.

Hata hivyo Dkt. Salandi amesema changamoto nyingine kubwa ni matunzokwa watoto ambapo kulikuwa na familia 106, zilikuwa na changamoto yamatunzo kwa watoto na kufan ya kufanya asilimia 32 hivyo kwenyeidara hiyo wameendelea kutatua changamoto na migogoro 334 ,ilifikakikomo kwa kufuata taratibu za kisheria ikiwemo polisi.

Diwani wa Kata ya Miyomboni ,Jeremiah Kisangai amesema utelekezaji watoto unasabishwa na wanaume kuingia kwenye mahusiano na kusabishamimba zisizotarajiwa kwa asilimia kubwa kama halmashauri zoezililishafanyika la kuwapitia na kupatikana kwa mashauri mengi zaidiya 300.

Kisangai amesema kuwa baada ya kuyapitia walibaini vitu vingi lakinikubwa halmashauri imejipanga kwenye maeneo ya vijiji kuna kamatizinazoshughulikia kukaa kila wakati kushughulikia kero hizo ilikupunguza matatizo hayo hususani Madiwani .