May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ushirikiano wa Tanzania, China kukuza Soko la Mazao ya Bahari

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

Waziri wa Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Shaban Omary amesema ushirikiano baina ya Tanzania na China unawezesha utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa buluu na utalii ambao unahusisha usafirishaji wa Mazao ya Bahari na Samaki.

Aidha amewashauri Watanzania wote nchini kufika katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kujionea na kutumia fursa
mbalimbali zilizopo ndani ya nchi na zile zilizopo nchini China.

Waziri Shaban ameyasema hayo Julai 4, 2023 katika hafla ya siku ya China (CHINA DAY) iliyofanyika kama programu moja wapo ya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dares Salaam (Sabasaba) valiyoanza Juni 28 hadi Julai 13, 2023 katika Viwanja vya Mwl. J.K.Nyerere Jijini Dares Salaam.

Waziri Shaban pia amesema kutokana na ushirikiano huo baadhi ya makampuni kutoka China yameanza kutengeneza vyumba ya kuhifadhia bidhaa (COLD
ROOM) ili kurahisisha usafirishaji wa Mazao ya Bahari na Samaki na kukuza uchumi wa bluu

Naye, Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amesena Wachina ni washirika wakubwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo na maadhimisho haya ya Sabasaba na
ujenzi wa eneo la biashara la Ubungo(Ubungo busterminal zamani)litakalo kuwa na Malls nyingi katika eneo hilo.

Naye Balozi wa Jamhuri ya China Chen Mingjian amesema maadhimisho hayo yameendeleza mahusiano mazuri yakibiashara na kitamaduni kati ya
Tanzania na China na Africa.