Na Mwandishi wetu ,Timesmajira.
NAIBU Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Michael Urio Leo (Diwani ) amemtembelea na kumlia hali mgonjwa Kalume Ally (41) na kuomba serikali, viongozi wa Serikali kujitokeza kwa wingi kumsadia matibabu na huduma za kibinadamu.
Mgonjwa huyo, Ally Kalume ambaye anasimamiwa kwa ukaribu na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Wa Dar es Salaam (DCPC), amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Kibasila No11,
Awali, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumuona Urio alisema Kalume yupo kwenye maumivu makali na kuuomba uongozi wa hospitali kumsadia kwa hali na mali.
“Nimefika wodini, nimebahatika kumuona ndugu yetu, kwa kweli yupo kwenye maumivu makali sana, ameniambia na nimemuona, ombi langu kwa uongozi wa hospitali ya Muhimbili tumsaidie ndugu yetu huku sisi tukiendelea kuiomba jamiii imsaidie kwa Hali na Mali, naamini tutafanikiwa” amesema Urio.
Amesema kuwa, anaomba Mawaziri, Wabunge, Madiwani na watu mbalimbali kujitokeza kumchagia.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi wa huduma za upasuaji Dk Rachel Mhavile amesema, mgonjwa huyo alipokelewa Agost 24 akitokea Hospitali ya Temeke na tayari ameshafanyiwa vipimo vyote.
“Tayari ameshachukuliwa vipimo vyote na tunangoja vipimo tuone tunaanzia wapi, kwa Sasa anapewa dawa za kutuliza maumivu , ” amesema Dkt. Mhavile kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Dk Mohammed Janabi.
Nae Mwakilishi wa Kamati ya kuratibu matibabu ya Mgonjwa huyo kutoka DCPC, Careen Mgonja, ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ukaribu wa Mgonjwa huyo katika kupatiwa matibau huku akiomba wadau na watu mbalimbali kuendelea kuchangia kupitia namba maalum ya aliyeteuliwa.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa