May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Umri huu mwanaume hupunguza kushiriki tendo la ndoa

Na Aveline Kitomary ,TimesMajira Online,Dar es Salaam

UKOSEFU ama upungufu wa nguvu za kiume ni ile hali ya mwanaume kutokuwa na uwezo wa kukamilisha kushiriki tendo la ndoa kwa ufasaha.

Tatizo hili linawakabili mamilioni ya wanaume duniani na limekuwa na athari nyingi kama vile kuvunjika kwa mahusiano na hata ndoa.

Kwa kadiri umri wa mwanaume unavyosonga mbele hasa wakati wa kuelekea uzee mzunguko wa damu katika mwili hupungua hali hiyo husababisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kupungua.

Hii huenda ikiwa ndio dalili kadhaa za ukomo wa uzazi kwa mwanaume lakini sio wazi kutokana na mbegu za mwanaume kuzalishwa kila siku tofauti na mwanamke ambaye hufikia ukomo wazi.

Kutokana na kupungua kwa shughuli za mwili tofauti na ujana huenda athari ikaonekana katika nguvu za kiume, Michael Anthony (63), anakiri kuwa madai hayo ni kweli kutokana na mabadiliko anayoyaona ukilinganisha na kipindi kilichopita.

“ N i k w e l i k a d r i u m r i unavyokwenda na viungo vya mwili vinaanza kuchoka tofauti na kipindi cha ujana,sasa hivi kuna vitu vingi siwezi kufanya kama zamani hasa haya magonjwa ya kuumwa mwili yanachangia kutokuwa vizuri.

 “Kwa tendo la ndoa nikilinganisha zamani na sasa naona kama nimeanza kuchoka na kwa hali hiyo sijawahi kwenda hospitali ila naendaga kwa wataalamu wa tiba asili kupata dawa za kunisaidia,” anaeleza.

Michael ni mmoja wa wanaume walio wengi ambao uwezo wao wa kushiriki tendo la ndoa umepungua wakati umri unasonga, kutoka ana hilo Jarida la Majira ya Afya lilimtafuta Daktari Bingwa wa uzazi kwa wanaume, ili kujua haswa ni nini kinatokea.

 NI LAZIMA UWEZO KUPUNGUA

Dkt. David Mgaya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili[1]Mloganzila, anasema kuwa zipo sababu zinazochangia uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kupungua kwa mwanaume kwa kadri umri unavyoenda mbele.

 “Ni dhahiri kuwa katika umri mkubwa mwanaume anahitaji muda mrefu wa kutosha wa kujiandaa wakati mwingine anahitajika kuguswa katika via vya uzazi ndio apate hisia, wakati mwingine kuweza kuhimili kufanya tendo moja kwenda lingine anahitaji muda wa kutosha.

 “Mwanume huyo wakati wa ujana wake alikuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa mara tatu au mara nne na zaidi ya hapo lakini utakuta anapunguza inakuwa mara mbili au mara moja kwa siku tatu na wakati mwingine mara moja hata kwa wiki kwa hiyo tendo moja la ndoa mpaka lingine inakuwa na muda mrefu.

“Akiwa kijana hisia zinakuja hata akisikia sauti au harufu au akiona tayari anaweza kushiriki lakini umri ukienda hawezi, tukihusisha nguvu za kiume na uzazi hata umri ukisogea kwa mwanaume uzazi huwa unaendelea tangu balehe inapoanza.

Anaongeza: “kwa sababu mbegu zinatengenezwa kila siku ila umri unavyosogea nguvu za kiume zinapungua ndio pale mwanaume anashindwa kusababisha ujauzito kwasababu yeye mwenyewe anashindwa kushiriki tendo la ndoa na unakuta moja wapo ya sababu homoni za ‘testosterone’ zinakuwa zinapungua kwa mwanaume ni pale nguvu za kiume zinapungua lakini mara nyingi uwezo wa kuzalisha mbegu upo lakini tendo la ndoa linamshinda.

Dkt. Mgaya anasema uwezo wa mwanaume kushiriki tendo la ndoa unaweza kuanza kupungua kuazia miaka 55 kwenda juu.

“ H a t u a y a u t u u z i m a inasababisha mishipa ya homoni ya ‘sterosid’ kushindwa kutanuka hii inaweza kupunguza nguvu, kingine ni utumiaji wa sigara na ulevi ulipindukia athari yake baadae ni kuharibu mishipa ya damu nguvu za kiume zinapungua,” anabainisha Dkt.Mgaya.

Anasema kuna sababu nyingine ambazo ni magonjwa yanayoshambulia mfumo wa damu kutokana na kuwa na mafuta mengi kwenye damu, hali hii inaweza kuziba mishipa midogo ya damu na kupunguza nguvu za kiume.

 “Katika mwili tunaweza kuzungumzia magonjwa ambayo yanaweza kufanya kupungukiwa na nguvu kama magonjwa ya moyo, presha ya kupanda, kisukari, magonjwa ya utu uzima, maumivu ya mgongo, kiuno na upasuaji au mionzi inaweza kusababisha mtu kupungua nguvu za kiume.

“Mfano kuna dawa za kutibu magonjwa kama presha zipo dawa ambazo mtu akizitumia nguvu za kiume zinapungua, dawa za magonjwa ya sukari, saratani ya tezi na saratani za aina tofauti zipo zinazopunguza nguvu za kiume.

“Kwa hiyo kama ni daktari anamtibu mgonjwa wake anaweza kumtahadharisha,”anafafanu Dkt. Mgaya.

Anaeleza kuwa matibabu ya upasuaji kama saratani ya tezi,sehemu ya chini ya kiuno inaweza kugusa mishipa ambayo inafanya uume kusimama na kusababisha tatizo la nguvu za kiume.

 WACHACHE HUJITOKEZA

Dkt. Mgaya anasema watu wenye tatizo hilo mara nyingi hawajitokezi ili kupata matibabu badala yeke wanakimbilia tiba za asili.

“Hapa kwenye kilinki yangu ninaweza kuona wanaume wanne hadi watano ambao wana umri mkubwa wakipata matibabu sasa idadi hii ni ndogo.

“Hili suala unajua wengi wanaona ni aibu kuzungumza watu wanaamini ikishatoka imetoka na hakuna njia au wengi wanaenda kutafuta tiba mbadala,” anasema Dkt. Mgaya.

MIGOGORA YA KIFAMILIA YATAJWA

Majira ya Afya, pia lilifanya mahojiano na wanasaikolojia kutaka kujua uhusiano wa kupungua kwa uwezo wa kushiriki tendo la ndoa na umri kusonga mbele. Christian Bwaya ni Mhadhiri wa Saikolojia, kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU) anasema saikolojia ni sehemu muhimu katika ushiriki wa tendo la ndoa lakini pia anakiri tatizo la kupungua kwa uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa wanaume ambao umri wao umeenda.

“Tukiacha saikolojia ya kwanza ni afya maana yake ni kwamba kadiri unavyoendelea kuwa mtu mzima mwili unachoka seli nyingi zinakufa kuliko zinazozalishwa, mishipa ya kusafirisha damu inachoka.

 “Lakini kisaikolojia tendo la ndoa linategemea akili inawaza nini na hamu ya kushiriki tendo kama imejengeka katika akili la sivyo uwezo utakuwa mdogo.

Anasema katika umri wa utu uzima akili ya mtu inakuwa ikitafakari maisha yake hali ambayo husababisha wengi kupata msongo wa mawazo.

“Umri wa utu uzima mtu anatafakari maisha yake wengi hupata msongo wa mawazo, wakati huu mwanaume kushiriki tendo la ndoa inakuwa changamoto kwani anawaza vitu vingi kama matatizo na hali ya majuto.

 “Hitilafu ya mahusiano kati ya mwezi wake, wanaume wengi wanaweza kuwa na changamoto za mahusiano, hali ya kuzoeana inasababisha kumwona wa kawaida, hivyo kukosa msisimko, hivyo kuweza kushiriki yaweza kuwa changamoto,” anabainisha Bwaya.

Msaikolojia huyo anasema sababu nyingine ni hofu inayowakumba ikiwa mtu mzima atakuwa na uhusiano na mwanamke mwenye umri mdogo.

“Mfano mtu mzima ana uhusiano na mtu mwenye umri mdogo kuliko yeye anakuwa na hofu ya kuweza kumudu tendo na unakuta anashindwa kufanya tendo au hata kuweza kupata madhara,” anaeleza

Msaikolojia Bwaya. A n a s e m a c h a n g a m o t o inayowakabili watu wazima ni kuwa na uwazi katika tatizo linalowakumba la kupungukiwa na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.

“Watu hawa wanaaibu kusema inachukua muda na mara nyingine hawaleti kama tatizo lake, watu wa namna hii wako wengi mtu anakuja kuulizia labda anasema ninarafiki yangu anatatizo lakini kumbe ni yeye hivyo kwa watu wazima ni ngumu kuja moja kwa moja hapa wapo wengi wanaoenda kutafuta tiba asili kama suluhisho.

 Daktari wa Saikolojia kutoka Cliniki ya Saikolojia ya AAR, Boniventure Balige, anasema mwanaume akiwa na msongo wa mawazo atakuwa hana uwezo wa kufanya tendo la ndoa kutokana na kitendo hicho kutegemea na fikra.

 “Kadiri tunavyokua miili yetu inakosa nguvu, kama unaakili imejaa stress unakosa uwezo wa kufanya ngono, ubongo unakataa kutokana na kile unachofikiri.

“mimi naamini kupungua nguvu inatokana na uwezo wa akili, kuna mwingine akiwa na mwanamke fulani hafanyi vizuri na akikutana na mwingine anafanya vizuri kwahiyo kinacholeta hamu ni uwezo wa mawazo,”anaeleza Dk Balige.

 TIBA ASILI MKOMBOZI WA WENGI

Awali katika mahojiano na Daktari wa Uzazi kwa Wanaume anabainisha kuwa watu wengi wanaopata matatizo ya nguvu za kiume hawafiki hospitali badala yake huishia kwa wataalamu wa tiba asili.

Na pia Msaikolojia Bwaya anadhibitisha kuna ukweli kuwa tiba asili imekuwa na nafasi kubwa kukimbiliwa kwa tatizo hilo.

 Kutokana na hilo Jaridi la Majira ya afya lilifanya mahonjiano na mwanaume mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Saimon anasema “Nilishawahi kuambiwa na marafiki zangu kama wanne hivi wakisema kuwa wanaishiwa nguvu wakati wanapokuwa wakishiriki tendo la ndoa na nilivyowauliza ni njia gani walipata msaada walisema kuwa walienda kwa wataalamu wa tiba asili wakawepewa dawa na zimewasaidia.

“Wanaume wengi hawafikirii kwenda hospitali kupata matibabu wakati mwingine ni kutokujua au kuogopa hata kwa ushauri wa kisaikolojia wanaona tiba asili ni muhimu na ni njia rahisi pia.

 Mtaalamu wa tiba asilia, Boniventura Mwalongo, anakiri kuaminika kwa tiba asili katika kutibu tatizo la uwezo wa tendo la ndoa.

Mwalongo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira anasema si wazee tu hukumbwa na tatizo hilo hata vijana wanaathirika pia kutokana na sababu mbalimbali.

 “Ni kweli nakubaliana umri au uzee ni hutua ya mwisho ya mwili wa binadamu, mwili na akili vinachoka na kupungukiwa, hilo ni jambo lisilo na pingamizi.

 “Na wapo tu watu wazima wengi wanakuja kueleza shida zao, sina idadi kamili ila ni wengi na wanapenda kuja kwetu kwasababu wako huru kueleza matatizo yao kwa wazi, wanaamini kuwa wanauwezo wa kupona.

“Mtu akipata ufumbuzi wa tiba asili anaamini kapata ufumbuzi wa kudumu, wengi wanaamini na kutumia dawa za asili.

Anabainisha kuwa hadi sasa hakuna tafiti zilizofanywa isipokuwa makadirio ya idara ya saikolojia ya Muhimbili inasema kuwa yapata watu milioni 300 ambao wana changamoto za athari za kisaikolojia zinazoathiri uwezo nguvu za kijinsia.

“Sababu ya kwanza ya watu kupenda tiba asili upatikanaji wake ni rahisi, hakuna madhara zikitumika kwa usahihi, ufanisi wake ukitofautisha na matibabu ya kisasa uwezo wa tiba asili ni pale sayansi inaposhindwa.

 MADHARA YA KUPUNGUA UWEZO

 Kwa mujibu wa Dk Mgaya madhara ya kupungua kwa uwezo wa kushiriki tendo la ndoa ni kupoteza kujiamini na kuwa na wasiwasi.

 “Kupoteza uwezo wa kuzalisha, hii haimaanishi kwamba wanaume wote wanaokosa watoto wamepungukiwa nguvu za kiume, hapana kunasababu nyingi,” anabainisha Dk Mgaya.

DALILI ZA KUPUNGUA UWEZO WA NGONO

 Dkt.Mgaya anasema dalili za kupungua uwezo wa kushiriki tendo la ndoa ni uume kushindwa kusisimama au kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa.

 “Kusimama na kushindwa kuingia ukeni au kushindwa kusimama kwa muda na kushindwa kuhimili tendo la ndoa.

 “Inaweza kutokea katika mara moja au mbili mwanaume akashindwa kufanya tendo la ndoa kabisa au kwa kiasi asichokitegemea lakini hii ya mara moja au mbili haimaanishi kuwa hana nguvu.

“Ikiwa ameshindwa moja kwa moja au tatizo la muda mrefu kusimamisha, kushiriki tendo la ndoa au kushindwa kuingia uke tunaweza kusema anatatizo la nguvu za kiume kwasababu tatizo limekuwa la muda mrefu,” anasisitiza Dkt Mgaya.