January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Umoja wa Kinamama wa Kiislamu wakoshwa na Banda la STAMICO

Na Penina Malundo,Timesmajira, Online

WANAWAKE wa Umoja wa Kinamama wa Kiislamu Tanzania, wametembelea Banda la Stamico na kuomba kushirikishwa zaidi katika mradi wa mkaa mbadala unatokana na makaa ya mawe ambao ni rafiki kwa mazingira.

Wametoa ombi hilo jana wakati walipotembelea Banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyomalizika kwenye VIwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mariamu Mtambo, amesema katika banda hilo wamevutiwa na mradi huo ambao wamehaidi kutumia katika uwekezaji.

“Tumefurahi kupita katika Banda hili,tumeona vitu mbalimbali miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na mkaa wa makaa ya mawe, hivyo tungeomba baada ya kuanzishwa kwa mradi huu tungependa kufahamishwa ili tuweze kujua jinsi tutakavyopata,”amesema

Kwa upande wake Afisa Masoko Mwandamizi wa STAMICO, Bilton Otto amesema wamefurahishwa na umoja huo kutembelea banda lao na kwamba ndani ya mwaka huu katika maonesho ya Sabasaba STAMICO imekuja kutangaza mtambo wa kisasa wa kusafisha dhahabu ambao una uwezo wa kusafisha kilo 480 kwa siku.

Mwenyekiti wa Jumuiya Wanawake wa Kiislamu nchini, Mariamu Mtambo akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Masoko Mwandamizi wa STAMICO, Bilton Otto kuhusuMkaa Mbadala wa Makaa ya Mawe utakaokuwa unazalishwa na STAMICO .

Amesema kwa Tanzania mtambo huo,ndio mtambo wa kisasa zaidi upo mkoani Mwanza na upo katika ubia kati ya STAMICO na watu wa Dubai.

Aidha amesema STAMICO wamekuja kuelezea umma juu ya mradi wao wa mkaa mbadala kwani ni rafiki kwa mazingira.

“Mwenyekiti na ujumbe wake umefurahi miradi yetu miwili na wamesema watatoa ushirikiana pindi miradi hiyo itakapoanza,”amesema