January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ujenzi wa Barabara ya Njambe-
Ndoga unaofanywa na TARURA Nyasa

Muonekano wa ujenzi wa barabara ya Njambe-Ndonga yenye urefu wa kilometa saba inayojengwa kwa gharama ya sh. milioni 69 ikijumuisha na ujenzi wa mitalo, daraja na makaravati, ujenzi huo unaofanywa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) wilayani Nyasa Mkoa wa Ruvuma. Kijiji hicho kitafikiwa na barabara hiyo kwa mara ya kwanza tangu Uhuru.
Mhandisi wa TARURA Wilaya ya Nyasa, Thomas Kitusi akizungumza na waandishi wa habari (hawap0 pichani) juu ya ujenzi wa mradi wa barabara ya Njambe- Ndonga yenye urefu wa kilometa saba ambayo ilikuwa haijawai kuchongwa tangu Uhuru.
Mhandisi Thomas Kitusi akielekeza namna barabara ya Njambe-Ndonga itakavyojengwa kwa kupigwa zege maeneo korofi ili iweze kupitika wakati wote wa msimu wa mvua na kiangazi, barabara hiyo hadi kukamilika itakuwa imegharimu kiasi cha sh. milioni 69 fedha za mfuko wa maendeleo.
Moja ya barabara ya rami iliyotengenezwa na TARURA wilayani Nyasa kwa fedha za maendeleo kutoka mfuko wa jimbo ambazo zilitolewa na Rais Samia Hassan Suluu kiasi cha sh. Milioni 500. RARURA Wilaya ya Nyasa wameweza kujenga barabara ya rami yenye urefu wa kilometa 1.5 chini ya mkandarasi Ovans. Picha zote na Cresensia Kapinga.