May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Udahili vyuo vya elimu ya ufundi waanza

Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma

BARAZA la Taifa la Elimu ya Vyuo vya Ufundi nchini (NACTE) limefungua dirisha la udahili katika vyuo vyote cya ufundi nchini kwa mwaka 2021.

Hayo yamebainishwa leo jijini hapa na Mkurugenzi wa Udhibiti ,Ufuatiliaji na Tathimini wa NACTE Dkt. Geofrey Oleke huku akisema dirisha hilo limefunguliwa leo kwa hiyo wahitimu wanaruhusiwa kuomba nafasi katika vyuo hivyo.

“Kwa mwaka huu udahili katika ngazi ya stashahada na astshaha umefunguliwa rasmi leo Mei 27,2021 hadi Agosti 14 mwaka huu katika awamu ya kwanza,hivyo Vyuo vinaruhusiwa kufanya maombi ya udahili kuanzia leo .” alisema Dkt Oleke

Amevitaka vyuo vyote nchini kuchagua waombaji wenye sifa huku akisema Agosti 15-20 mwaka huu vyuo vitachagua waombaji wenye sifa na kisha Agosti 21 hadi Septemba 3 mwaka huu majina ya waombaji waliochaguliwa yatawasilishwa NACTE kwa ajili ya uhakiki.

Alisema,majina yaliyochaguliwa na kuhakikiwa na NACTE yatatangazwa na vyuo husika Sept 16 ,2021 kwa ajili ya kuanzia masomo.Novemba Mosi 2021.

Aidha amesema,waombaji wa program za afya kwenye vyuo vya Serikali watatuma maombi yao moja kwa moja kupitia tovuti ya baraza kuanzia Mei 27 -Juni 14 mwaka huu na majina yatatangazwa Agosti 22 ,2021.
Amevielekza vyuo vyote vya Elimu ya ufundi vitakavyopeleka maombi kwa ngazi ya stashahada na astashaha kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi katika programu wanazoziomba.

Aidha Baraza hilo linawashauri waombaji kuhakikisha wanaomba kwenye vyuo vilivyopo kwenye kitabu cha muongozo huku akisema watakaoomba vyuo hivyo ndio watakaochaguliwahuku akisema Muongozo huo unapatikana tovuti ya www.nacte.go.tz.