January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ubunifu wa kuzuia wizi katika banda la kuku wawavutia wengi maonyesho ya ubunifu

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MWANAFUNZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ngazi ya Diploma Irene Wilbard ametengeneza bunifu ya kuzuia wizi au wadudu waharibifu wa kuku kwenye mabanda kwa kuweka ishara ambayo itamjulisha mfugaji kwamba kwenye banda lake kuna kitu kinaendelea.

Akizungumza jijini Dodoma kwenye maonyesho ya wiki ya ubunifu amesema,ameamua kufanya bunifu hiyo kutokana na matukio mwngi ya wizi wa kuku au kuku kuliwa na wadudu kwenye mabanda na hivyo kumrudisha nyuma muhusika (nmfugaji).

“Nimetengeneza banda la kuku ambalo lina usalama wa kutosha kwa mfugaji wa kuku,ambapo kama kutatokea kitu ambacho siyo cha kawaida kwamba kuna mwizi au mdudu anayekula kuku kaingia bandani,kuna kifaa nimefunga ambnacho nimkiunganisha na simu,hivyo kitapiga alarm ya kuonysha kwamba kuku wapo kwenye hatari ya kuibwa au kuliwa na wadudu kama vile nyoka na wadudu wengine.”amesema Irene na kuongeza kuwa

“Mradi huu ni mzuri na ninaamini watu wengi hasa wafugaji wa kuku wataupenda kwani kuku wao sasa watakuwa salama.”

 Kwa mujibu wa Irene,mradi huu utaenda kutatua changamoto nyingi katika jamii lakini pia kuwasaidia vijana wengi watakaoshawishiwa na mradi huo kujifunza na kujiajiri kwa kuwafungia watu kwani naamini wengi wataupenda.

Ametumia nafasi hiyo kuwaasa vijana kupenda na kuingia kwenye masuala ya Sayansi na Ubunifu kwani kuna fursa kubwa za ajira.

“Kwenye la Sayansi na Teknolojia ndiko kuna fursa nyingi za ajira,vijana wanapohitimu masomo wanaweza kujiari wenyewe pasipokutegemea ama kusubiri ajira za Serikali,hii ni fursa lazima vijana tuamke na tuitumie ,itatuwezesha kuendesha maisha yetu lakini pia kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.