May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ubungo yaongoza ujenzi wa madarasa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Ubungo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala ,amesema Halmashauri ya Ubungo wameshika nafasi ya kwanza ujenzi wa madarasa ya Sekondari .

Mkuu wa Mkoa Amos Makala aliyasema hayo katika ziara yake Wilayani Ubungo leo wakati alipofanya ziara ya kikazi kuangalia Maendeleo ya ujenzi wake .

“Nawapongeza Ubungo kwa kufanya vizuri mnashika nafasi ya kwanza ,Madarasa yamekamilika 27 kati ya Madarasa 81 madarasa 54 yapo hatua za mwisho kwa asilimia 90 ,Wilaya ya Ilala wao wamekuwa wa pili asilimia 70 ya ujenzi waliofikia “alisema Makala .

Makala alisema ziara yake ni ya kikazi dhumuni la ziara hiyo kuangalia ujenzi wa madarasa ya Wanafunzi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuelekeza pesa za ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 600 katika mkoa huo ambapo Ubungo wameupiga mwingi na majengo yake yana ubora wapo tayari kupokea Wanafunzi .

Alisema Ubungo sawa na mtoto aliyewai kutembea kifua mbele madarasa ya UVIKO pia walikuwa wa kwanza wakati pesa Halmashauri zote wamepewa siku Moja .

Alitumia siku hiyo kuwapongeza Madiwani wa Wilaya ya Ubungo Kkwa usimamizi mzuri ,Meya ,Mkuu wa Wilaya Ubungo Khenry James na Mkurugenzi wao.

Aliwataka Viongozi wa chama Ubungo kusemea kazi ya utekekezaji wa Ilani inayofanywa na Serikali ya awamu sita ambayo inaongoza Dola kwa ajili ya kuwatumikia Wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Khenry James alisema Wilaya ya Ubungo wanajenga madarasa 81 ya Sekondari yaliokamilika madarasa 27 madarasa 54 yapo hatua za Mwisho Ujenzi wake.

Alisema ziara hiyo ya mkuu wa Mkoa ametembelea Shule ya Sekondari Kiluvya na Mbenzi Luis fedha za Ujenzi walizokabidhiwa shilingi Bilioni 1 .6 pesa ya Rais, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya walishakagua wamejilidhisha majengo yana ubora.