Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mercy Sila, amewataka wanawake wote wajasiriamali kujiunga na chama hicho, ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza jijini i Dar es Salaam leo Julai 6,2023 kwenye viwanja Vya maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa, maarufu kama Sabasaba, Mwenyekiti huyo amesema wanawakaribisha wanawake wote wajasiriamali kujiunga na chama hicho, huku akitaja moja ya faida ya kujiunga, kitamuwezesha mwanamke mjasiriamali, bidhaa zake kutambulika ndani na nje ya nchi.
Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akifanya hususan katika suala zima la uboreshaji wa mazingira ya kufanyia biashara, jambo ambalo limewasaidia wanawake wengi na vijana wajasiriamali.
” Kwanza kabisa napenda kumshukuru Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akifanya hususani katika uboreshaji wa mazingira ya kufanyia biashara,hivyo sisi kama wanawake pamoja na vijana wajasiriamali imetupa urahisi katika biashara zetu,” amesema Mercy.
Pia ametoa wito kwa wanawake wote Tanzania Bara na Zanzibar kujitokeza kwa wingi kujiunga na TWCC, kwani faida zake ni nyingi huku akielezea kuwa uhitaji ni mkubwa kwani wapo watu wengi wanajiunga hata katika maonesho hayo ya Sabasaba wapo wengi.
Aidha amemshukuru Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, kwa kuendelea kuwashika mkono wanawake hao huku akisisitiza kuwa wao kwa umoja wao hawatamuangusha na wataendelea kufanya vizuri ili kuhakikisha chama hicho kinafika mbali zaidi.
Ameongesa kuwa wana mkakati wa kuhakikisha wanawake wote wafanyabiashara walio katika chama hicho wanaunganishwa na wadau ili kufikia kiwango cha kumiliki viwanda vikubwa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Usimamizi wa Uvushwaji Bidhaa Kutoka Tanzania kwenda nchini Malawi, katika Chama hicho, Rose Leonard, ambaye ni mfanyabiashara jijini Mbeya akiwa ameshukuru Waziri Mkuu Mstaafu Wa Mizengo Pinda, baada ya kutembelea na kuona bidhaa zao na kuonesha kuwatia moyo wanawake.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba