January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tume ya Ushindani yazitaka kampuni zinazoungana kuwasilisha maombi

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online

TUME ya Ushindani Tanzania(FCC) imezitaka kampuni za kibiashara zinazotaka kuungana kuwasilisha maombi ya usajili katika ofisi hiyo huku ikisisituza maombi hayo ni lazima yawe yamezingatia Sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa.

Akizungumza katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimatafa DITF yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam Mtendaji Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC), William Erio amesema kabla ya Kampuni hizo kupeleka maombi zinapaswa kuhakikisha zinasoma Sheria husika sambamba na kufanya utafiti ili maombi yao yaweze kupokelewa .

Alisema kuwasilisha maombi katika Tume hiyo yaliokamilika na kuzingatia Sheria itasaidia Kampuni hizo kamailisha hatua za uwekezaji kwa haraka zaidi.

“FCC imejipanga kuhakikisha usajili wa Kampuni za kibiashara zinazotaka kuungana unafanyika kwa mujibu wa Sheria maombi yanayowasilishwa mapema yatafanyiwa maamuzi haraka ili hatua zinazofatwa ziweze kuendelea”alisema

Na kuongeza kuwa FCC ikiridhika na maombi yaliopelekwa itatoa kibali kwa Makampuni hayo kuendelea na Muunganiko “alisisitiza Erio

Akitaja mambo ambayo ayaruhusiwi kwa mujibu Sheria ya Makampuni ni pamoja na kutokuozi soko anaeleza kufanya hivyo kuna athari zake huku akiweka wazi Sheria inaelekeza kutokumiliki zaidi ya asilimia 35 ya soko katika bidhaa moja.

Pia Makampuni hayo ayapaswi kuwa na makubaliano yanayovunja au kukiuka na kuondoa Ushindani pamoja na kuwaathiri wateja.

Alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu alitoa maelekezo hivi karibuni wakati akimuapisha Makamu wa Rais, na badae alipokuwa akiwaapisha mawaziri kuhakikisha uchumi wa Viwanda unaendelea kuwa vizuri.

Alibainisha kuwa katika kipindi cha serikali ya awamu ya sita tayari Tume hiyo imeishaanza kufanya utekelezaji wa suala hilo ambapo jumla ya maombi 19 yameishashugulikiwa katika kikao kimoja.
.
“lengo letu ni kuhakikisha kila maombi yanayokuja yanatolewa maamuzi haraka ili hatua zinazofuatwa ziwezi kutekelezwa tukifanya hivyo tutaweza kuimarisha viwanda, ajira, tutaleta mitaji, Teknolojia ambayo itawezesha Viwanda na uchumi wa nchi kukua “alisema

Katika hatua nyingine alisema soko la bidhaa bandia katika nchi Bado ni tatizo huku akisisitiza uchumi wa Viwanda uwezi kuwa mzuri kama utaruhusu au kuachia bidhaa bandia katika soko.

Alisema uwepo wa bidhaa bandia una madhara makubwa ikiwemo kuwakimbiza wawekezaji wapya wanaotaka kuja kuwekeza nchini.

“Ni jukumu letu kuhakikisha kuwa bidhaa bandia azina nafasi kwani zinamadhara mengi katika jamii na kwa taifa kwa ujumla pamoja na kusababisha ukwepaji kodi.

Aidha alitoa rai kwa watu wanaojishughulisha na kuleta na kutoa bidhaa bandia katika nchi kuacha mara moja kwani FCC imejipanga kuhakikisha inaweka watendaji wake katika mipaka na bandarini hakuna bidhaa bandia inayoweza kuingia nchini .