
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mwigulu Lameki Nchemba ameiagiza kamati ya Usalama ya Mkoa wa Rukwa kufuatilia kwa kina sakata la Mzee wa miaka 60 anaeishi halmashauri ya wilaya ya kalambo mkoani Rukwa la kuibiwa mtoto mmoja wa kiume baada ya mke wake kujifungua mapacha katika hospitali ya wilaya ya Nkasi.
Mzee huyo akieleza mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mzee huyo amesema jambo lake halijashughulikiwa toka mwaka jana mpaka kufikia siku ya leo.
Akihutubia mamia ya watu katikaTarafa ya Kasanga Halmashauri yaWilaya ya Kalambo leo Marchi 10,2026 Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Mwigulu Lameck Nchemba ndipo ameiagiza kamati ya usalama ya Mkoa wa Rukwa kushughulikia suala la kuibiwa kwa mtoto wa mzee huyo ili haki iweze kupatikana.

More Stories
JNHPP: Ndoto ya Nyerere yatimia,Rais Samia apongezwa
Rais Samia aagiza wakuu wa Mikoa kujiandaa na udhibiti wa Athari za El Nino
InnoIP Tanzania yazinduliwa kuimarisha ulinzi wa ubunifu