May 2, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tume ya Madini yawapiga msasa wachimbaji wadogo wa madini

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Timu ya wataalam waandamizi wa Tume ya Madini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Mhandisi Henry Mditi wameendelea kutoa mafunzo kwa wamiliki wa migodi, wachimbaji wadogo wa madini na wasimamizi wa baruti kuhusu usimamizi wa afya, usalama, baruti na sheria za madini katika eneo la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Katika mafunzo hayo ambayo awali yamezinduliwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba mada zilizotolewa ni pamoja na sheria ya madini na kanuni kuhusu eneo tengefu la Mererani na uchimbaji salama migodini.

Mada nyingine ni pamoja na utunzaji wa mazingira migodini na usimamizi wa baruti migodini.

Wakizungumza katika nyakati tofauti wadau wa madini waliohudhuria mafunzo hayo wameipongeza Tume ya Madini kwa utoaji wa elimu safi na kushauri elimu kuendelea kutolewa kwenye maeneo mengine yenye shughuli za uchimbaji wa madini nchini.