April 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tulia Trust yakabidhi mifuko 400 ya saruji shule za msingi na sekondari

Na Esther Macha, TimesmajiraOnline,Mbeya

KATIKA kuhakikisha kuwa mazingira ya miundombinu ya shule za msingi na Sekondari Jijini Mbeya yanaendelea kuimarishwa na kuwa na ubora Taasisi ya Tulia Trust imekabidhi msaada wa mifuko mifuko 400 ya Saruji kwa shule za msingi na Sekondari Jijini hapa.

Hayo ni mwendelezo wa Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt .Tulia Ackson na Spika wa Bunge na Rais umoja wa mabunge duniani katika kutimiza ahadi zake kwa wananchi.

Msaada huo umekabidhiwa leo,Machi 26,2024 na Ofisa Habari Taasisi ya Tulia Trust ,Joshua Mwakanolo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Spika wa Bunge ikiwa ni jitihada zake za kuhakikisha kuwa miundombinu ya Shule inakuwa imara na kuwafanya watoto kusoma katika mazingira rafiki ya shule.

Mwakanolo amesema kuwa utoaji Saruji katika shule ni sehemu ni kutimiza ahadi ambapo amesema kuwa lengo ni kuboresha miundombinu ya elimu kwa shule za msingi na kuutaka uongozi wa shule na kata wa Mlimani kutumia Saruji katika matumizi yaliyokusudiwa na isitumike nje ya matumizi .

“Ndugu zangu wananchi na viongozi mtakaokwenda kusimamia Saruji hii tunawaomba ikafanye kazi iliyokusudiwa na isiwe ikawa fursa ya kuchepusha na kwenda sehemu nyingine isiyolengwa katika kazi iliyokusudiwa hili tulielewe ndugu zangu “amesema Mwakanolo .

Akizungumza wakati wa kupokea Saruji hiyo Mkuu wa shule ya msingi Mlimani,Jane Mwaisumo alimshukuru Dkt.Tulia Tulia kwa msaada huo wa Saruji wa mifuko 200 na kusema kuwa kuna shule nyingi katika Jiji la Mbeya lakini kwa upendo wake ameiona shule ya msingi Mlimani.

Hata hivyo Mkuu huyo shule ametoa shukrani zake kwa wafanyakazi wa Tulia Trust kutokana na kujitoa kwake na kuwaomba wadau mbalimbali wa elimu kuhakikisha kwamba wanajitoa katika kuchangia sekta ya elimu .

“Tuna wadau wengi Jijini hapa hivyo tuombe wamuunge mkono Mbunge wetu wa Jimbo la Mbeya mjini katika harakati zake za jitihada za kuhakikisha kuwa anaboresha miundombinu ya elimu iliyopo Jijini hapa, tunahitaji shule zetu ziwe na mazingira mazuri hivyo wadau wenye uwezo wa kuchangia wajitoe “amesema Mkuu huyo wa Shule.

Honolata George ni Ofisa elimu kata katika kata ya sinde amekiri kwamba wamekuwa na changamoto ya madarasa katika shule ya msingi ya mlimani hivyo msaada wa saruji wa mifuko 200 na kwenda kutatua changamoto ya uhaba vyumba vya madarasa katika katika shule hiyo.

“Tumekuwa na changamoto kubwa sana ya upungufu wa vyumba vya madarasa mbunge wetu Dkt.Tulia ameona atupatie shule yetu ya Mlimani kwa kutupatia mifuko 200 kwani utatusaidia kutatua changamoto hii katika shule yetu hii “amesema .

Hata hivyo baada ya kukabidhi mifuko hiyo ya saruji katika shule ya msingi mlimani Taasisi ya Tulia Trust iliendelea kufika katika Shule ya sekondari Dkt.Tulia iliyopo katika kata ya Iyunga na kukabidhi mifuko ya Saruji 100 pamoja na kukabidhi Mil.2 kwa ajili ya ukarabati wa mabweni katika shule hiyo na kumalizia kukabidhi mifuko ya Saruji 100 kwa shule ya sekondari Itende iliyopo kata ya Kalobe.