November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tulia Marathon kurindima Mei 2024

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya Tulia Trust imeandaa mashindano ya Mbeya Tulia Marathon kwa msimu wa nane ambayo yanatarajiwa kuanza Mei 10 mpaka 11 mwaka huu lengo likiwa ni uboreshaji miundombinu ya elimu, afya pamoja na uwezeshaji kiuchumi kwa wananchi.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa taasisi ya Tulia Trust, Joshua Edward akifafanua jambo kwa waandishi wa habari

Hayo yamesemwa Januari 27,2024 na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Tulia Trust, Joshua Edward wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mashindano ya Mbeya Tulia Marathon ambayo yatafanyika kuanzia Mei 10 mpaka 11 mwaka huu Jijini Mbeya katika uwanja wa Sokoine ambapo huu ni msimu wa nane toka yalipoanzishwa.

Edward amesema kuwa taasisi ya Tulia Trust kwa muda mrefu imekuwa ikijihusisha na uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya elimu na afya.

“Yataanza kuanzia saa 12.00 asubuhi ambapo Mei 10 kutafanyika mbio fupi ambazo ni Mita 100,Mita 200,Mita 400,Mita 800, na Mita 1500 ambapo Mei 11 yatafanyika mashindano ya mbio ndefu ambazo ni Km 5,Km10,Km,21, pamoja Km 42 ikiwa ni pamoja na kukabidhi zawadi kwa washindi wote wa riadha kwa siku hizo mbili,”.

Pia amesema kuwa katika mashindano hayo kutakuwa na vituo kadhaa vya kuuzia namba za usajili ili uweze kushiriki kikamilifu katika kuwania ushindi huo wa Mbeya Tulia Marathon 2024.

Mratibu wa mashindano ya Tulia Marathon,Lwiza John akionesha medali za washindi kwa waandishi wa habari

“Katika haya mashindano tunakaribisha wajasiliamali mbali mbali kutumia fursa hii katika kufanya biashara zao bila gharama yeyote pamoj ili waweze kukuza vipato vyao “amesema.

Mratibu wa Tulia Trust Marathon ,Lwiza John amesema kuwa katika mashindano hayo suala la zawadi litakuwa pale pale kwa washiriki wa uwanjani na wa mbio za barabarani.

Joyce Mwakifwamba ni Ofisa Michezo Jiji la Mbeya amesema kuwa taasisi hiyo ni msaada mkubwa kwani imekuwa ikiangalia kila nyanja lakini bado katika eneo la michezo haijaacha kwenye ambapo kila mwaka wamekuwa wakikimbia ili kujenga afya zao.

“Ninaachoomba wakazi wa Mbeya tumuunge mkono Dkt.Tulia kwa sababu lengo lake ni nzuri ambalo ni kuimarisha miundombinu ya elimu na afya,”amesema Ofisa Michezo huyo.