May 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mashabiki wa Simba na Yanga Bungeni kukiwasha uwanja wa Jamhuri


Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

WABUNGE na watumishi wa Bunge wanaoshabikia timu za Simba na Yanga wanatarajia kuuwasha moto katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma huku   mashabiki na viongozi wa timu hizo wakitambiana vikali.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Spika Bungeni jijini Dodoma,Mwenyekiti wa Timu ya Soka ya Bunge Festo Sanga amesema ,pambano hilo ni moja ya mchezo mingi ambayo itachezwa katika bonanza lililodhamini wa na benki ya Azania.
“Katika bonanza hilo kutakuwa na mchezo 23 ambayo yote itachezwa kwa muktadha wa timu za  Simba na Yanga .”amesema Sanga
Aidha amesema,mgeni rasmi katika bonanza hilo atakuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) ambapo Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wanatarajiwa kushiriki .
“Kuandaliwa kwa bonanza ni maono ya Spika Dkt.Tulia ambapo lengo kubwa ni kuinarisha mahusiano baine ya watani wa jadi,wabunge ,taasisi mbalimbali pamoja na kuimarisha afya zetu.”amesema Sanga
Kwa upande wake Msemaji na Afisa Habari wa Timu ya soka ya Yanga Ally Kamwe amesema wapo pamoja na timu ya wabunge wanaoshabikia Yanga huku akisema ni furaha kwa Yanga kujumuika kwenye bonanza hilo huku akiwahamasisha wabunge kujipanga na kufanya vizuri katika mpambano huo.
“Kesho tunafunga ofisi Jangwani tunahamia Dodoma ,hatutaki kucheza na mtu ,maana sisi ikishawekwa logo ya Yanga mahali ,shughuli hiyo tunaichukulia kwa umuhimu mkubwa ,kwa hiyo wabunge nendeni mkautwange susi tupo nyuma yenu.”
Akizungumza kwa niaba ya Timu ya Simba Ally Shatry amewaasa mashabiki wa Simba wajitokeze kwa winginkatika pambano hilo huku akisema Simba hawanaga shughuli ndogo.
Mkurugenzi Mhazini na Masoko ya Mitaji wa Benki ya Azania Gilbert Mwandamile  amesema Benki hiyo imedhamini bonanza hilo ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya michezo ikiwemo mpira na jezi.
“Benki ya Azania imeona ni vyema watunga sera wadhamini pambano hilo ili wapate fursa ya kujenga mahusiano na makundi mengine kupitia michezo.”amesema Mwandamile