January 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tulia aahidi kuboresha miundombinu mfereji Sinde

Na Esther Macha,Timesmajira,Online,Mbeya

WANANCHI wa Kata ya Sinde Jijijni Mbeya,wamemuomba mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt.Tulia Ackson kuwaboreshea miundombinu ya mifereji ya maji hususan katika mito ili kuepukana na hadha ya mafuriko ya mara kwa Mara inayohatarisha usalama wao.

Mbunge mbeya mjini afanya ziara kata ya Sinde kutembelea miundombinu ya mifereji ya kata ya Sinde eneo la Ilolo baada ya kutoa malalamiko yao kwa mbunge mvua inaponyesha.maji yanajaa ndani ya nyumba za wakazi hao

Wamesema hayo leo wakati wa ziara ya mbunge huyo ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na barabara na mifereji ya maji katika jiji la Mbeya.

Mkazi wa Sinde Thomas Mwangama amesema kuwa mfereji huo wa Sinde wamesumbuka kwa muda mrefu maji yanayopita kwenye mfereji huo yanatoka eneo la Mwanjelwa na uwanja wa ndege ya zamani pamoja na shule ya sekondari Sangu.

Amesema kuwa nyumba zao zipo hatarini kubomoka hasa kipindi hichi cha mvua kwani maji yakijaa yanajaa ndani ya nyumba zao hivyo waliomba kujengewa mifereji ambao itasaidia maji yanayopita kwenye mifereji hiyo yasiweze kuingia kwenye nyumba zao.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Sinde,Fanuel Kyanuala amesema kuwa kata ya Sinde kwa mjini ipo mjini hivyo inahitaji mifereji mingi na imara zaidi.

Kwa upande Naibu Spika ambaye ndiye mbunge wa jimbo hilo Dkt.Tulia Akson amewataka wakazi wa kata ya Sinde A kujitokeza kusafisha mfereji wa ulioziba takakata wakati suluhu inatafutwa ya kutengeneza mfereji huo ambao unaunganisha mifereji saba ya Jiji la Mbeya.

Dkt.Tulia amesema kuwa mfereji huo unaunganisha mifereji saba ya Jiji la Mbeya na kwamba uchafu huo umezidi hivyo ni vema wakati inatafutwa suluhu ya kudumu mfereji huo ukasafishwa kwanza ili kuondoa taka zote zilizoziba.

“Niwaombe wana Sinde kuwa watulivu kipindi hichi ambacho tunatafuta suluhu ya kudumu pia niwaombe wote tukubaliane na kuweka nguvu hivyo tukutane wote hapa kesho kuanzia saa mbili asubuhi ambapo tutanzia upande wa juu kusafisha mfereji na sasa hivi naelekea ofisi ya mkurugenzi kuomba vifaa kwa ajili ya kusafishia huu”amesema Dkt.Tulia.