Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kurahisisha maisha ya kimawasiliano kwa watalii na wananchi kwa ujumla kwa kufikisha huduma za mawasiliano ya Intaneti kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Dkt.Tulia ameyasema hayo jijini hapa leo,Mei 18,2023 wakati alipotembelea Banda la Shirika hilo lililopo kwenye viwanja vya Bunge katika maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yenye lengo la kuonesha shughuli zinazofanywa na taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.
Amesema kuwa TTCL kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuvitangaza vivutio vya utalii vya Tanzania .
Aidha amesema kuwa uwepo wa huduma za mawasiliano zinaimarisha shughuli za ulinzi na usalama kwa wataliiwakiwa mlimani kupitia mamlaka husika jambo ambalo ni kivutio cha kuchochea uchumi wa kidigiti.
“Nitajipanga vizuri niende mlima Kilimanjaro kwasababu nitakuwa na uhakika wa mawasiliano mpaka nitakapo kuwanafika kileleni na kuwepo kwa Intaneti mlima Kilimanjaro kwakweli kutakuwa hakuna uongo uongo kwasababu ukifika pale maana yake ndiyo upige video tujue umefika ama hujafika,
“Kwahiyo nawapongeza sana kama mmeweza kufika katika mazingira yale ya kilele cha juu zaidi Duniani kwa mlima ambao umesimama nawapongeza sana”amesema Dkt.Tulia.
Vilevile amewapongeza TTCL kwa huduma yao nyingine ya kupeleka mawasaliano nyumbani ametaja kitendo hicho ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya uchumi wa kidigiti kwani itamrahisishia mawasiliano kila mtanzania.
Pamoja na hayo aliipongeza Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuleta maonesho hayo katika viwanja vya Bunge ili wabunge waone wenyewe yanayoendelea katika maeneo yao ya uwakilishi.
“Kwani nimejionea hapa leo zoezi la anuani za makazi ambayo yalianza mapema mwaka jana na sasa tumefikia sehemu ambayo yule ambaye tayari amesajiliwa anuani yake anaweza kuipata kiganjani kwa kutumia aina yoyote ile ya simu jambo ambalo ni zuri sana,”amesema Dkt Tulia
Kwa upande wake Meneja biashara TTCL, Dodoma Leyla Pongwe ametaja lengo la shirika hilo kuwepo katika maonesho hayo kuwa ni kuwaonesha wabunge mikakati ambayo wamejiwekea katika kusaidia serikali kufikia uchumi wa kidigitali mpaka kufikia mwaka 2025.
“Katika shughuli ambazo tumeleta kuonesha hapa kwanza tumeweza kurahisisha utalii baada ya kuweza kufikisha mawasiliano katika miaka 61 ya uhuru tumewezesha kufikisha mawasiliano katika kilele cha mlima kilimanjaro(Uhurupeak) na hiki ndiyo kilele cha Afrika mashariki kwasababu ukisimama pale juu unauwezo wa kuona Afrika mashariki yote.
“Zamani mtalii alikuwa akipanda juu anakuwa hapatikani mpaka atakapokuwa ameshuka ila kwasababu tumewezesha mawasiliano mtalii ataweza kupatikana kila kituo ambacho anafikakwasababu tumewawekea WiFi pamoja na mkongo na atakuwa anapatikana,”amesema Pongwe.
Pia Pongwe ameeleza huduma nyingine wanayoonesha katika maonesho hayo ni huduma ya Faiba Mlangoni kwako ni huduma ambayo mtanzania ataletewa mpaka nyumbani kwake bure na yeye atakachotakiwa kufanya ni kulipia kifurushi chake cha mwezi ambacho sasa hivi tunajua kwamba ilikufikia uchumi wa kidijitali lazima uwe na Intaneti iliyoimara ilikuwezakifanya mawasiliano ya kimtandao.
“Lakini tumekuja kuwajulisha wabunge ukiwa na mtandao wa faiba unaweza kuwasaliniana na kufanya vitu hata ukiwa uko mbali mradi tu unamtandao wa TTCL hivyo unaweza kufuatilia nyumba yako kwa kuona kwa kuangalia kupitia Application ya simu,”amesema.
Pamoja na hayo Pongwe amezungumzia mkongo wa Taifa ambapo amesema wameweza kufikisha mkongo katika mipaka yote ya nchi na sasa wameanza kutoka nje ya Tanzania ili kufikisha mawasiliano ya faiba kwenda katika nchi za Jirani za Afrika Mashariki pamoja na zinazozunguka Tanzania .
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini