April 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TTCL kuifanya Tanzania kuwa nchi kiongozi,ukuaji wa uchumi wa kidjitali

Na Penina Malundo,Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Bodi Shirika la Mawasiliano la Taifa TTCL Zuhura Muro amesema TTCL inauwezo wa kuifanya Tanzania kuwa nchi kiongozi kwa ukanda wa Afrika Shirika na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC ),sio tu kiteknolojia bali kutokana na kasi yake ya ukuaji wa uchumi wa kidjitali.

Akizungumza hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,alisema anaaamini kuwa Shirika hili likiendelea kufanya vizuri katika mawanda ya uchumi wa kidjitali kwa Tanzania utazidi kupanda kwa kasi ya juu.

Amesema kutokana na dunia ya sasa ipo kidjitali ndio maana TTCL hadi sasa imepiga hatua katika kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kutumia magari kutangaza utalii hali iliyofanya watanzania kwa sasa kuona picha mubashara ya watalii wakipanda mlima wa Kilimanjaro na kuona hali yake.

“Kwa hatua kubwa TTCL imepiga hatua kubwa sana kwa nguvu walizoweka hasa katika mkongo ni kuunganisha nchi kila kona na katika kuunganisha nchi yetu itakuwa na maingiliano ya tija zaidi na kuwezesha uchumi wetu kwenda mbele zaidi,”amesema.

Aidha amesema nchi itakapounganisha nchi nyingine kidigitali itaweza kusaidia kuongeza pato la mapato ya fedha za kigeni na uchumi kuzidi kukua.”Nimepata fursa ya kutembelea banda letu leo na nimefurahi sana kutokana na unyeti wa Shirika hili kwa taifa letu hasa wanapozungumzia uchumi wa kidjitali,”amesema na kuongeza

“Tutauza ubunifu , Teknolojia nje ya nchi kupitia TTCL huku Watanzania wataona jinsi ambavyo shirika linavyonda na uwezo wa kuifanya Tanzania ikawa nchi kiongozi sio tu kiteknolojia lakini kiuchumi katika ukanda wetu ,kiusalama na kiutamanduni pindi itakapouza digitali,”amesema.

Amesema kukuza huduma za kidigitali ni maendeleo yaliyopo katika Shirika hilo kwani shirika linaweza kuwa muhimili mkubwa katika kuhifadhi data za wafanyabiashara hata wale wa kati ambapo data zitakuwa salama.

“TTCL ni Kituo Kikuu cha Data ambacho kinaunganisha vituo yao vyote katika nchi na kwa mashirikiano mazuri ambayo wamekuwa nayo na Shirika la umeme (Tanesco) wanahakikisha data za wateja wao zitakwenda vizuri Umeme utakuwepo na Wananchi wanataweza kuzipata,”amesema.

Amesema TTCL pia inatoa huduma ya call center kwaajili ya mashirika mbalimbali na wafanyabiashara mbalimbali badala ya mashirika kuingia gharama sisi tunauwezo kwa sababu tunamajengo na Teknolojia na wataalamu wa kuendesha vituo vya kupigia simu(call center).

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika hilo la TTCL,Peter Ulanga aliwakaribisha wananchin katika Banda lao kupata huduma ya Mawasiliano.”Sisi ndio tumekabidhiwa kuendesha mkongo wa Taifa ambao unaunganisha nchi saba lakini tunampango wa kuunganisha nchi ya nane ambayo ni nchi ya Kongo Mashariki,”amesema na kuongeza

“Pia tunajaribu kubadilisha mtazamo wa matumizi ya internet Tanzania badala kuwa na ya vifurushi tutaona iwe ya unlimited kwa kutumia fayber,sisi TTCL tunaubeba uchumi wa kidigitalo kama nguzo muhimu ya uchumi hapa nchini na tunafanya kazi bega kwa bega kuhakikisha kwamba uchumi huu wa kidigitali utawatoa unatutoa hapa tulipo na kwenda katika maeneo makubwa ya Maendeleo katika nchi yetu,”amesisitiza