Na Esther Macha,Timesmajira,Online , Mbeya
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt.Edwin Mhede amesema kuwa mamlaka hiyo imefanikiwa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka mwaka 2014/2015 na kuongezeka kutoka trilion 10.67 mpaka kufikia trilioni 17.87 katika mwaka wa fedha 2019/2020.
Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano wameweza kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuiwezesha serikali kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na huduma za kijamii.
Dkt.Mhede amesema hayo jana wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha tathmini utendaji kazi wa idara ya kodi za ndani kikao hicho cha siku nne(4)kinachofanyika katika ukumbi wa NHF Jijini Mbeya ambacho kimeshirikisha Mameneja wa Mikoa yote 30 ya kikodi ya Tanzania Bara,na mameneja wasaidizi .
Aidha Kamshina Mkuu huyo amesema kwamba makusanyo hayo ni ongozeko la wastani wa kutoka Bilion. 850 zilizokuwa zinakusanywa kwa mwezi wakati serikali ya awamu hii inaingia madarakani hadi kufikia wastani wa, trillion 1.5 kwa mwezi ikiwa ongozeko la asilimia 76 kwa mwezi.
Akielezea ogozeko hilo Dkt. Mhede amesema kuwa makusanyo hayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na jitihaa za hati za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli .
Amesema kwamba TRA imekuwa ikipewa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuiongezea uwezo wa kiutendaji kwa kuboresha sheria na mifumo ya usimamizi wa kodi ,kudhibiti nidhamu na uadilifu katika kuzuia mianya ya ukwepaji kodi kwa ujumla.
Akifungua kikao kikazi hicho Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alisema mafanikio makubwa yanayokuwepo kati ya TRA na Serikali na vyombo ya dola yanafanya kuwepo na moyo wa kulipa kodi kwa wananchi na kwamba kuweza kufakiwa kwa kiasi kikubwa .
Aidha amesema ukweli ni kwamba uadilifu unatakiwa katika chombo hiki nakwamba wakati fulani kukiwa na mkwama wakati wa makusanyo ya kodi huwa kunasababishwa na kukosekana na uaminifu na kuwa mara nyingi kukiwa na madili mengi suala la ukusanyaji kodi lazima liwe hafifu .
Akizungumzia utoaji wa elimu kwa walipa kodi Kaimu Kamshna wa Idara ya kodi za ndani (TRA),Abdul Mapembe amesema kuwa mara nyingi wakiitisha semina wanaokuja ni wale ambao hawahusiki sio na wakiulizwa wahusika husema wanakuwa na kazi nyingi .
“Kwa hiyo imekuwa ni mpaka wafuatwe mmoja mmoja na kumfuata mmoja ni kazi ndo maana tuna vipindi kwenye Tv na radio lakini idara hii ina watu wanazunguka Tanzania nzima kwa hiyo elimu tunatoa sana kwa walipa kodi wetu na kuwa elimu wanayo ya kutosha”amesema Kaimu Kamishna huyo.
Mwisho.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapato