May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TPF-NET Arusha waandaa Iftari kwa ajili ya watoto yatima

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mtaandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha katika kuhakikisha unaendelea kuyakumbuka makundi mbalimbali katika jamii umetoaa misaada katika kituo cha Watoto yatima Ummu Aisha kilichopo jijini Arusha huku wakibainsha kuwa mbali na misaada hiyo wameandaa halfa ya iftari kwa ajili ya Watoto wa kituo cha Ummu Aisha.

Akiongea katika halfa ya kukabidhi vitu mbalimbali Mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake Mkao wa Arusha Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema wao kama sehemu ya Jamii wamekuwa na utaratibu wa mara kwa mara kufuturisha makundi tofauti tofauti katika jamii ambapo amebainisha kuwa kipindi hiki wamefika katika kituo hicho kwa ajili ya kutoa misaada.

SSP Zauda amebainisha kuwa Jambo ambalo wamelifanya katika kituo hicho ni kuandaa iftari na kufuturisha Watoto katika kituo hicho cha Ummu Aisha ambapo amebainisha kuwa wametumia fursa hiyo kutuo elimu ya ukatili wa kijinsia na Usalama Barabarani ili kuwajenga katika kujikinga na ajali Barabarani.

Ally Issa Meneja wa kituo cha kulea Watoto yatima Ummu Aisha licha ya kulishukuru Jeshi la Polisi kwa namna ambavyo wamekikumbuka kitu hicho kwa kutoa misaada mbalimbali ambayo amebainisha kuwa itawasaidia Watoto katika kituo hicho huku akiomba jamii nyingine kuyakumbuka makundi ya wahitaji katika jamii.