Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Mara
WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua biashara ya Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) ya usambazaji wa mafuta ya petroli na dizeli pamoja na bidhaa zitokanazo na mafuta hayo.
Uzinduzi huo ulifanyika kwa Waziri Kalemani kuzindua pia vituo vya mafuta zaidi ya 10 nchini vinavyomilikiwa na TPDC ambavyo vitatoa huduma ya kuuza mafuta kwa wananchi chini ya usimamizi wa shirika hilo.
Zoezi la uzinduzi wa vituo hivyo Kitaifa umefanyika mjini Musoma mkoani Mara alipozindua vituo viwili cha Musoma na Tarime vilivyopo mkoani hapa akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Subira Mgalu na watendaji wa wizara yake.
Amesema, mwezi huu wameanza na vituo saba na kwamba, vituo vyote nchini vitakuwa chini ya usimamizi wa TPDC huku akisema kuwa vituo vyote vinapaswa kusimamiwa vyema na kutoa huduma kwa ufanisi unaotakiwa kwa wananchi.
Amesema kuwa, kupitia uzinduzi wa vituo hivyo viwili vya Mkoa wa Mara vingine vyote vilizinduliwa rasmi nchini huku akisisitiza sera inataka kupeleka nishati vijijini.
Waziri Kalemani amesema,uzinduzi wa vituo hivyo ni hatua mojawapo ya kusogeza huduma za nishati karibu kwa wananchi ambao wanapaswa kunufaika na huduma hizo, kwa kuzitumia katika shughuli za kujiletea maendeleo kama ambavyo sera inaelekeza.
“Nishati siyo umeme peke yake, mafuta ni nishati, gesi ni nishati, upepo ni nishati, lakini tumeanza kupeleka nishati vijijini ni katika harakati za utekelezaji wa azima ya Serikali ya kufikisha huduma hizi za nishati kwa wananchi ziwasaidie kupiga hatua za kimaendeleo,”alisema.
Aliongeza kuwa, zoezi la usambazaji wa gesi asilia majumbani linakuja na kwamba utekelezaji wake unaanza mwakani, alisema wametoa maelekezo kwa wasambazaji wote wa gesi za mitungi bei ifanane isiwe kubwa, alisema wameunda timu ya kufuatilia na kufanya uratibu ili bei hiyo iwe ndogo isiwaumize wananachi.
Amesema,wataleta gesi ya kwenye mabomba ambayo bei yake itakuwa na punguzo la asilimia 40 na kwamba, haitakuwa na gharama kubwa ikilinganishwa na bei ya mkaa, hivyo akawataka wananchi kujiandaa kutumia nishati hiyo ambayo itakuwa rahisi na kila mmoja atamudu gharama ya matumizi yake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dkt.James Mataragio amesema kuwa, Serikali iliingia kwenye biashara hiyo kwa mfumo wa soko huria kwa kuunda kampuni tanzu na kwamba ilifanikiwa kununua na kujenga vituo mbalimbali nchini ikiwemo Kituo cha Makuyuni na Makumira mkoani Arusha, Segera na Muheza mkoani Tanga.
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito