Na Mwandishi wetu Timesmajira online
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk Faustine Ndugulile, ametoa miezi mitatu kwa Shirika la Posta Tanzania (TPC) pamoja na Shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL) kumaliza migogoro yao ya mali na majengo huku akitaka hadi ifikapo Septemba mwaka huu mali hizo ziwezimegawanywa tayari.
Dkt Ndugulile ametoa agizo hilo Mkoani Dar es salaam jana wakati akifungua kikao kazi cha siku tano cha viongozi wa Shirika la Posta kilichowakuta Mameneja mikoa, watendaji wakuu chenye lengo la kufanya tathimini ya utendaji wa kazi .
Amesema apo awali mashirika hayo yalikuwa ni Shirika moja na badae yalikuja kugawanywa na kuwa Taasisi tofauti hivyo zipo baadhi ya mali na majengo bado ayatambuliki ni mali ya Taasisi ipi .
” Tulishatoa maelekezo kwa Mashirika hata kukaa pamoja na kugawana mali na kwa zile zenye shida ya kugawanywa basi watushirikishe Wizara na msajili wa hazina ili kuweza kutatua “amesema Dkt Ndugulile
Amesema mali zote za kila Taasisi zinapaswa kutagazwa katika gazeti la Serikali na kueleza kuwa hapo itakuwa ni utimisho la kutambua nani anamiliki mali gani .
Katika kikao hicho Dkt Ndugulile amewataka watendaji wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) kufanya kazi kwa umoja na mshikamano ili Taasisi hiyo iweze kufika mbali zaidi na kusisitiza kuipa thamani nembo ili iweze kuwa kivutio kwa wateja
“Ili Taasisi iweze kufika mbali ni muhimu kuwatumia watendaji waliomaliza muda wao kujifunza vitu mbalimbali na kushirikiana nao ili kuleta mabadiliko”amesema
Na kuongeza “Shirika la Posta lazima liwe na mtanzamo , Muonekano na katika utendaji wa kazi na Huduma”amesisitiza
Amebainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha Shirika la Posta linakuwa katika mfumo wa kidigitali na kuwa kitovu cha Biashara katika mtandao.
“Kuna maboresho makubwa tumefanya katika Shirika hili katika kipindi cha miezi nane ya Uongozi wangu tangu ni teuliwe na Rais Samia Suluhu Hassan la Posta kwa sasa linakwenda vizuri ili liweze kuwa kielelezo na kuangazia fursa”amesema
Kwa upande wake Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Macrice Mbodo amesema katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia April hadi kufikia hivi Sasa Taasisi hiyo imefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia 70 tofauti na awali.
“Kwa Mwaka huu tumejipanga kuzalisha asilimia 20 hadi 30 zaidi ya kile ambacho tulikipanga katika mwaka uliopita”amesema Mbodo
Naye Mkuu wa Kitengo Cha Usimamizi wa Ubora kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Haruni Lemanya amelitaka Shirika la Posta pamoja na watendaji wake kushirikiana ili kuhakikisha huduma ya Posta inasonga mbele na kufika mbali kwa kuweka mikakati bora .
More Stories
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25