January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TOMA yazinduliwa Msigwa asisitiza weledi kwa vyombo vya habari mtandaoni

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amesema kwasasa vyombo vya habari mtandaoni vingi vinasumbuliwa ni weledi kwa baadhi kuzusha habari zisizokuwepo.

Kutokana na hayo Msigwa amewataka wadau wa masuala ya habari na wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia weledi katika utendaji kazi wao hasa katika kipindi hiki cha Mapinduzi ya teknolojia kwa kuhakikisha wanazingatia maudhui yanayoendana na taaluma hiyo.

Msigwa ametoa wito huo jijini hapa leo,Februari 10 ,2023,wakati akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari,mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kabla ya kuzindua taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni (TOMA) .

“Sisi tunapaswa tujitahidi kujitofautisha na hao ili tulinde taaluma yetu na Serikali sio kwamba haioni juhudi za vyombo vya habari inaona na ndio maana imetoa uhuru wa kutosha kila mmoja kuanzisha na kumiliki chombo cha habari ila changamoto inatokea namna gani ya kuchuja kipi kiende hewani na kipi kisiende kulingana na maudhui yake,”amesema Msigwa 

Msigwa amesema kuwa  kutokana na kukuwa kwa matumizi ya TEHAMA imerahisisha habari kufika kwa jamii kwa haraka sana hivyo vyombo vya mitandaoni imekuwa tegemeo kama chanzo kikuu cha habari kwa haraka.

“Tasnia ya Habari ipo mikononi mwa vyombo vya habari Mtandaoni, kwa sasa vyombo vya habari Mtandaoni imekuwa nguzo kubwa kwa sekta ya habari nchini ila nitoe angalizo kwa sababu kadiri zinavyoongezeka inaonekana kama weledi wake unapungua hivyo niwatale TOMA kuhakikisha waandishi wa habari mtandaoni wanakuwa na uelewa mkubwa juu ya machapisho wanaotuma mtandaoni,

“Hicho ndicho kitakachotufanya tuaminike na jamii ni  lazima tuangalie maadili ya uandishi wa habari yanasema nini, ni lazima tuangalie sheria za nchi yetu zinasema nini, hatuwezi kuwa waandishi wa habari za mtandaoni kwa kujikita tu kwenye kuzua taharuki, kuvunja sheria au kuchonganisha jamii na jamii au jamii na serikali,

“Tumetoka tulipotoka vyombo vya habari vikimilikiwa na wanasiasa na wafanyabiashara, akija mmiliki anasema weka hiki usiweke hiki,tuacheni kutumika, hapo ndipo heshima yetu itakuwepo, fanya kazi yako kwa weledi”.Â