Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
TIMU ya mpira wa miguu ya Under 20 imenyakuwa taji la kombe la Champion vijana kwa kuwafunga Under 17 kwa mikwaju ya penati 5-4 kwenye mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mzimuni, Dar es salaam.
Michuano hiyo ya kata Mzimuni ilidhaminiwa na Kampuni ya Alpha Tanganyika Flavour Limited inayojishughulisha na uchakataji wa samaki.
Mara baada ya mchezo huo wa fainali, Mkurugenzi wa kampuni ya Alpha, Alpha Nondo amesema kuwa lengo la kudhamini michuano hiyo ni kutaka kuwapa fursa vijana kuonesha vipaji vyao.
Mbali na hilo lakini pia Nondo alimsifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha kujali michezo nchini na kutoa uhuru kwa watanzania kufanya biashara.
“Lengo la kuanzisha michuano hii ni kutaka kuibua vipaji vya vijana na huku ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia katika kuinua sekta ya michezo nchini,” amesema
Katika mchezo huo wa fainali, Afisa Habari wa zamani wa klabu ya Yanga, Antony Nugaz ndio alikuwa mgeni rasmi ambapo aliwapongeza waandaaji wa michuono hiyo kwa kuwaleta vijana kuwa kitu kimoja.
Amesema kuwa michuano kama hiyo inaubua vipaji na kuleta ukaribu baina ya watu katika jamii.
More Stories
Rais Samia atia mkono mchezo wa masumbwi Tanzania
Chino bingwa mpya wa IBA Intercontinental Championship
Mnzava apania kuwapeleka vijana Simba na Yanga