January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Timu 193 Jimbo la Lipa Wilayani Chunya kushiriki  ‘Kasaka Cup’

Na Rose Itono,Timesmajira,Online

TIMU zaidi ya 100 za Jimbo la Lupa Wilayani Chunya Mkoani Mbeya zinashiriki mashindano  ya Ligi ya Kasaka Cup na kugawiwa vifaa mbalimbali vya michezo.

Akizungumzia mashindano hayo Mbunge wa Jimbo la Lupa ambaye ndiye muandaaji wa mashindano hayo  Masache Kasaka alisema mshindi wa kwanza atajinyakulia sh milioni moja

Amesema  mshindi wa pili atajinyakulia sh 500,000 huku mshindi wa tatu akiambulia sh300,000 huku timu zote  193 zitakazoshiriki ligi hiyo zitagawiwa jezi.

Amesema ligi hiyo ambayo ameizindua rasmi jana itamalizika mwezi Oktoba kwa washindi kijinyakulia zawadi zao”,”Kasaka Cup’ 2021 itaziwezesha time hizo kujijengea uzoefu wa kushiriki ligi mbalimbali sambamba na kujenga miili yao kwani michezo ni afya,”amesema