May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo waja na njia ya kumuweza mkulima kuzalisha kidijitali

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo imekuja na njia ya kijigitali ya kumrahisishia mkulima kujifunza namna ya uzalishaji wa mazao bora kwa njia ya mtandao ambapo inatoa mkopo wa simu janja kwa wakulima ambao hutanguliza pesa kidogo ili waweze kumudu gharama za kupata simu hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kujifunza kilimo mtandaoni kupitia simu  za mkononi,Meneja Mauzo na usambazaji wa Tigo mkoa wa Mbeya Ronald Richard amesema,kwa kutumia simu janja (Smart phone) amesema,mkulima anaweza kufanya kazi zake za kilimo kisasa zaidi na kuongeza uzalishaji.

“Tumeamua kuja na bidhaa hii kwa ajili katika maonyesho haya ya Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya kwa ajili ya wakulima na wananchi wote kwa ujumla ambayo inapatikana kwa kwa mkopo ambapo mtu anatanguliza pesa kidogo anachukua simu kisha anaendelea kulipia shilingi 1000 hadi 1500 mpaka mteja anapomaliza deni lake .”amesema Richard

Meneja huyo amewaasa wakulima na wananchi kwa ujumla kutumia maonyesho hayo ya Nane Nane kujipatia simu hizo huku akisema baada ya maonyesho huduma hiyo itapatikana katika maduka yao ya Tigo.

Aidha amesema kuwa kabla ya kuanza kulipia malipo hayo ya kila siku mteja anatakiwa kutanguliza kiasi cha shilingi 70,000 hadi 90,000 kulingana na simu anayohitaji mteja.

“Njia hii ni rahisi kwa wananchi wengi hususan wakulima kuweza kumiliki simu janja ukizingatia simu huuzwa kwa bei ghali na hivyo wakulima wengi kushindwa kumudu gharama hizo.”amesisitiza

Hata hivyo kwa upande wake mkulima aliyezungumza na vyombo vya habari baada ya kununua bidhaa hiyo kutoka Tigo Abdul Said amesema,njia hiyo ni rahisi hususan kwa wakulima wadogo ambao hawawezi kununua bidhaa hiyo kwa mkupuo.

“Tunaishukuru sana kampuni ya Tigo kwa kuja njia hii ambayo inaonekana kutujali sana wakulima hasa sisi wa chini ,kwani kwa ktumia simu hizi tunaweza kujifunza mambo mengi tandaoni yanayohusiana na kilimo na hivyo kutusaidia katika kuzalisha mazao bora na kwa tija.”amsema mkulima huyo